Ujenzi wa njia zinazo elekea kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kuna njia nyingi zinazo elekea katika malalo ya Atabulfadhil Abbasi (a.s) hasa zile zinazo tokea mji mkongwe, kutokana na wembamba wake pamoja na upitaji wa magari kwa shida katika barabara hizo sambamba na ubovu wake, ambazo hutumiwa zaidi na mazuwaru pamoja na wenye maduka, mafundi wanaofanya kazi katika kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kazi ya kuweka tofali ndogo ndogo katika barabara hizo. Kazi hiyo imetanguliwa na kazi za awali ambazo ni:

  • - Kufanya upembuzi yakinifu na kubaini njia zinazo takiwa kufanyiwa ujenzi huu.
  • - Kuchukua vipimo maalum vya ukubwa wa eneo linalo takiwa kufunikwa kwa tofali hizo ndogondogo.
  • - Kuondoa tofali zilizo kuwepo mwanzo na kuzipeleka nje ya mji.
  • - Kusawazisha njia hizo kwa kuziba sehemu zinye mashimo.
  • - Kuweka tabaka la kifusi peke yake na kukisawazisha.

Baada ya kumaliza kazi hizo ndio uwekaji wa tofali ndogo ndogo zilizo tengenezwa katika kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanza, pamoja na kuweka miferenji ya maji ya mvua na kuyaelekeza katika njia kuu ya maji. Tunapenda kusema kua kitengo cha uangalizi wa kihandisi ni miongoni mwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya vinavyo fanya kazi mfululizo kila siku, na kimesha fanya kazi nyingi za ujenzi katika maeneo ambayo yanasaidia kuboresha huduma kwa mazuwaru wa Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: