Waziri wa nyumba na makazi: Tunaunga mkono ushirikiano uliopo kati ya Atabatu Abbasiyya na taasisi za serikali

Maoni katika picha
Waziri wa nyumba na makazi Ustadh Bankin Rikani amesisitiza kua wizara yake inaunga mkono ushirikiano uliopo kati ya Atabatu Abbasiyya na taasisi za serikali katika utekelezaji wa miradi inayo saidia sekta mbalimbali za kiraia.

Ameyasema hayo alipo tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha akatembelea maeneo mbalimbali huku akiwa amefatana na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), akasikiliza maelezo kuhusu huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya, na kumbainishia kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inatumia nguvu kubwa katika kuendesha miradi ya kutoa huduma, mchango wake uko wazi namna inavyo watumikia wananchi”.

Hospitali ya rufaa Alkafeel ni moja ya sehemu alizo tembelea waziri, akasema huu ni mradi wa aina yake na msaada kwa taasisi za serikali, akasisitiza kua: “Sisi katika wizara yetu tunafanya kazi na kila taasisi inayo toa huduma kwa raia, na tunaisaidia kwa kiwango tutakacho weza, hasa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: