Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wafanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya maombolezo ya kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni na pande la Mtume Mtukufu Fatuma Zaharaa (a.s), kwa kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kupitia mradi wa Arshu Tilaawah na kushiriki wanafunzi wa mradi wa (Ri’ayatul Alawiyya liqiraa-atul-Iraqiyya) ambao upo chini ya Atabatu Alawiyya tukufu.

Qur’ani imesomwa kwa sauti nzuri sana iliyo ingiza unyenyekevu katika nyoyo za wasikilizaji, mazuwaru na wote walio kuwepo walifuatilia kwa karibu usomaji wa Qur’ani, mazingira ya kiroho yalitawala kwa kukutana utukufu wa Qur’ani na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wasomaji walikua ni: Muhammad Twaaiy, Abu Raaidu Jaabiri, Sayyid Yaasi Muhana na Hussein Maqdamiy kutoka Iran.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya miradi mingi ya Qur’ani, muiongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, unao lenga kunufaika na vipaji vya vijana wa kiiraq katika usomaji wa Qur’ani, na kudhihirisha vipaji hivyo katika ulimwengu wa kiislamu, sambamba na kuviendeleza kwa kufuata utaratibu maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: