Maoni katika picha
Shughuli ya kufunga ratiba ya hema la Skaut ilihusisha mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni kuswali Dhuhuraini kwa jamaa pamoja na kusoma dua maalumu za swala hizo, kisha wanafunzi wakasogea karibu na jukwaa na hafla ikafunguliwa kwa kisomo cha Qur’ani tukufu, halafu ukafuata ujume elekezi kutoka kwa Sayyid Mussawi mtumishi wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, alieleza mambo mengi na akawaombea mafanikio ya kukamilisha sarari yao ya kutafuta elimu, akawaambia kua anatarajia wamefaidika na siku walizo kaa kwenye hema, bila shaka wamezitumia vizuri chini ya mafundisho ya Dini yetu tukufu ya kiislamu na maelekezo ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), akawahimiza wayafanyie kazi waliyosoma wawapo vyuoni na majumbani, na wawe mabalozi wa kuyafundisha katika jamii.
Pia kulikua na ujumbe wa wanafunzi walio shiriki katika hema hilo, wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuwapa nafasi hii adhimu ya kujumuika pamoja na kupewa mafundisho ya kitamaduni na kimaadili, wameomba jambo hili liendelee katika vipindi tofauti ndani ya mwaka mzima, kwani lina faida kubwa kwao ya kuwafanya watumie vizuri kipindi cha likizo.
Hali kadhalika hafla ilipambwa na kaswida kuhusu kuwapenda maimamu wa Ahlulbait (a.s) na taifa la Iraq, na mwisho wanafunzi wakapewa vyeti vya kushiriki katika hema, baada ya hapo wakaelekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumshukuru mbele ya kaburi lake takatifu.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu husimamia na kufanya program za aina mbalimbali ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya, zinazo lenga kusaidia tabaka la wanafunzi kwa ajili ya kutilia mkazo mafundisho ya Dini tukufu ya kiislamu kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), pamoja na kujenga uzalendo wa kulipenda taifa lao.