Katika msimu wa nne wa likizo za shule: Mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomi wa kiiraq umeanza kufanya warsha zake za kimaadili…

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani ambacho kipo chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya kinafanya warsha kwa wanafunzi wa mradi wa kuandaa wasomaji wa kiiraq, katika msimu wa nne wa likizo, zaidi ya wanafunzi (100) kutoka mikoa tofauti wanashiriki.

Mkuu wa utekelezaji mradi huu Ustadh Muhammad Ridhwa Zubaidiy tumeongea nae kuhusu swala hili, amesema kua: “Kipindi cha likizo za nne ambacho pia ni kipindi cha nne cha mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomi wa kiiraq, mradi unaolenga kulea vipaji vya wairaq na kuviendeleza, tumeanza warsha chini ya mkakati uliowekwa na mradi, mwaka huu tumeanza na hatua muhimu kwa kuchagua wanafunzi wenye viwango vya juu na kuwapa semina ya kuwajengea uwezo moja kwa moja tarehe (11/2/2019), kutokana na viwango vilivyo pangwa mwaka huu, ambavyo vimefikiwa na Maahadi nyingi pamoja na taasisi za Qur’ani za hapa Iraq”.

Akaongeza kua: “Washiriki wa semina hii wamewekwa katika madarasa matano (5) ambayo ni: (darasa la Shekh Abdulbasit Muhammad Abduswamad, Shekh Muhammad Swidiq Minshawi, Shekh Shahata Muhammad Anuur, Haafidh Ismail, Shekh Mahmudu Ali Banna na madarasa zingine), kipindi hiki kimetumika kuwapa masomo ya kumalizia pamoja na kufanya kongamano la wanafunzi na walimu wao”.

Kumbuka kua mradi huu ni miongoni mwa miradi mizuri ya Qur’ani, unasimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya wakufunzi mahiri kutoka ndani na nje ya Iraq, unalenga kutengeneza kizazi cha wasomaji bora wa Qur’ani tukufu watakao endeleza usomaji kwa utaratibu bora na wakisasa, mradi huu unalenga wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kwa kutumia kipindi cha likizo za majira ya joto (kiangazi) kuandaa wanafunzi wengi na kuhakikisha wanakua na kiwango kizuri cha usomaji ndani ya kipindi cha miezi miwili takriban katika hatua ya kwanza ya mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: