Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye warsha iliyo fanyika ndani ya Atabatu Abbasiyya na kushiriki jopo la waandishi wa Alkafeel, miongoni mwa nukta alizo sisitiza Mheshimiwa ni:
- - Lugha ya kiarabu ni miongoni mwa lugha hai, kwa bahati mbaya inaanza kudhofika kwa sababu watu wake hawaipi umuhimu unayo stahiki.
- - Lugha inahitaji mzungumzaji na mwandishi, na inahitaji mpenzi na mlinzi.
- - Qur’ani tukufu imetuhifadhia lugha hii, tunatakiwa tujitahidi kulinda uzuri wake.
- - Tunatatizo katika maandishi ya zamani, inawezekana vijana wetu hawajui kwa sababu ya kuchukulia mambo juu juu na uchache wa kujisomea.
- - Yatosha kuangalia baina ya uhalisia wa lugha ya kiarabu na lugha inayo zungumzwa hivi sasa (mitaani).
- - Mtu anaweza akapatia irabu katika maneno, hilo sio tatizo, tatizo ni kuielewa lugha ya kiarabu vilivyo, kama isipo fundishwa vizuri itakuja kukosa baadhi ya vionjo vyake.
- - Wana nahau wana aina inaitwa majazi, maana ya majazi; mtu anatumia neno katika mahala ambapo sio pake.
- - Lugha ya kiarabu inavionjo hivyo, kuna vita ya majazi, baadhi wanasema: hakuna majazi, sehemu zote maneno yanatumika kwa maana yake halisi.
- - kwa hakika vionjo vya majazi mtu yeyote anayependa lugha humpa ladha.
- - Tunahitaji kurudi katika lugha ya kiarabu asilia, tuzidishe kusoma kiarabu halisi bila kuingiza lahaja wala kuruhusu maneno ya watu wengine yakatuharibia lugha yetu.
- - Tunapo angalia Qur’ani na kusoma Nahju Balagha tutaona ukaribu uliopo kati ya maneno ya kiongozi wa waumini (a.s), hata katika kitabu cha Swahifa Sajjaadiyyah, utaona ukaribu wa ujengaji wa sentensi na maneno, usomaji wa vitabu hivyo unasaidia kuimarisha uwelewa wa mtu na siri za kiarabu.
- - Kuhimiza uandishi, mtu hujieleza kwa maneno au kwa maandishi, maandishi hubaki hata baada ya mwandishi kufariki na huendelea kuwafundisha watu wengine, uandishi ni njia bora zaidi.
- - Kuzingatia misingi ya uandishi, mtu anaweza kuangalia alicho andika mwaka jana na anacho andika hivi sasa.
- - Kunamaendelea makubwa katika sekta ya uandishi hivyo inahitajika kujisomesha na kujiendeleza, hautakiwi kutosheka na kitu mwanzoni mwake hasa utakapo ambiwa kuwa kina tatizo.
- - Hali ya kawaida ni kwamba mwanaadamu haumbi kitabu, bali hujifunza kidogo kidogo hadi akaweza kuandika kitabu.
- - Lengo la kuongea ni kubainisha makusudio yako kwa ulimi, hili ni jambo muhimu zaidi, baadhi ya wakati nafasi huwa ndogo na unatakiwa kubainisha mambo, itakubidi utafute njia ya kubainisha ujumbe wako kwa ufupi, nayo ni mashuhuri zaidi kwa Mtume na kiongozi wa Waumini (a.s), kuongea maneno mafupi lakini yanaujumbe mkubwa.
- - Mwanaadamu muongeaji husema makusudio yake, na msikilizaji anaweza asieliwe vizuri, hivyo hatakiwa kuhukumu kitu hadi atakapo elewa makusudio yake, anatakiwa kuizowesha nafsi kua mzungumzaji na wala sio kua msikilizaji.
- - Mtu anatakiwa ajifundishe kutoka kwa Maimamu watakasifu (a.s), walikua na ufasaha wa hali ya juu, na Imamu Zainul-Aabidina (a.s) anaupekee wake katika ufaswaha na adabu, hakuna yeyote aliye weza kukosoa maneno ya Maimamu.
- - Tunapo angalia mitandao ya mawasiliano ya kijamii, tunaona namna watu wanavyo andika na wengine wanavyo kosoa, utamaduni wa wengi sio mzuri, maandishi yao yamejaa makosa pamoja na kutoeleweka madhumuni yao, bali kuna maneno yasiyo pendeza.
- - Mtu anapoangalia maandishi huhisi jambo fulani, lakini kwa sasa asilimia kubwa ya maandishi hayawakilishi uhalisia.
- - Kukithirisha uandishi katika mitandao kutapunguza ari ya watu kuandika na kujifunza, wakati zaka ya elimu ni kuifundisha, lazima ufundishe wengine, unapokua ni mtu mwema unaweza kufundisha wengine hata baada ya muda mrefu kupita.