Maoni katika picha
Kulikua na ujumbe wa Maahadi uliowasilishwa na mkuu wa Maahadi Shekh Hussein Turabi, alisisitiza umuhimu wa kalamu katika kutunza maarifa kwa mujibu wa Qur’ani tukufu na hadithi za Ahlulbait (a.s).
Naye Shekh Hussein Asadiy akabainisha kua: “Waandishi ya kielektronik wa Alkafeel wanafanya kazi ya kalamu kwani wana mtandao maalumu wa kielektronik unao itwa Alkafeel, hupokea makala mbalimbali na kuzisahihisha kilugha, kinahau, kibalagha na fani zingine, kisha huziwasilisha katika kamati wa wataalamu ambayo huzigawa sehemu tatu, sehemu ya kwanza hukataliwa, nayo nizile ambazo hazikupata kiwango cha ubora, na zingine huandikwa katika mtandao wa facebook ya Alkafeel na telegram na zingine huandikwa katika mtandao wa Alkafeel, sehemu ya kwanza huandikwa na kuhidadhiwa katika mtandao wa Alkafeel, huwekwa pia katika facebook na kwenye telegram, kwa ajili ya kuboresha kazi hii kamati inayo husika na uandishi imeanzisha kundi la telegram kwa jina la: (Familia ya waandishi wa Alkafeel), kwa lengo la kukusanya waandishi na kuwasiliana nao kupitia kundi hilo la telegram kwa ajili ya kuwashajihisha zaidi, vikao hivi vinasaidia kujuana baina yao na kubadilishana uzowefu, pamoja na kuangalia changamoto wanazo kutana nazo ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao kwa ajili ya kuboresha kazi hii, lengo letu ni kutangaza maarifa ya Dini kwa ujumla na maarifa ya Ahlulbait (a.s) kwa namna ya pekee kupitia uandishi huu ulioanza miezi kumi na moja iliyo pita, hadi sasa zimesha wekwa katika mitandao makala (800) au zaidi ya idadi hiyo ndani ya miezi kumi au zaidi”.
Naye Ustadh Ali Khabbaaz kiongozi wa idara ya habari ya Atabatu Abbasiyya tukufu aliongeza kwa kusema kua: “Waandishi wa Alkafeel ni waandishi wa umma wanategemewa pande mbili, upande wa kwanza ni upande wa sekta ya habari, na upande wa pili ni kuwapa moyo watumishi wetu wapya”, pia akaelezea namna ya uandishi na akatoa mifano mingi katika maelezo yake.
Tunapenda kusema kua Maahadi hufanya nadwa kila baada ya muda fulani kwa ajili ya kujadili mazingira ya elimu za kielektronik, na kutatua changamoto wanazo kutana nazo.