Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanya kongamano na maonyesho ya pili ya ubunifu…

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio yaliyo patikana katika kongamano na maonyesho ya kwanza ya ubunifu, Atabatu Abbasiyya imetangaza kufanyika kwa awamu ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Karbala ni chemchem ya misafara ya kielimu na wasomi) litakalo anza tarehe (20 hadi 22 Machi 2019m) sawa na mwezi (12 hadi 14 Rajabu 1440h) ambazo ni siku za kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s) kwa kushirikiana na umoja wa wabunifu wa kiiraq.

Tumeongea na Ustadh Jawadi Hasanawiy ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na maonyesho hayo, amesema kua: “Katika kuendeleza mafanikio yaliyo fikiwa katika kongamano na maonyesho ya kwanza uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu unafanya kongamano na maonyesho ya ubunifu awamu ya pili kwa kushirikiana na umoja wa wabunifu wa kiiraq, kongamano hili ni miongoni mwa matukio mengi yanayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya wananchi wa Iraq pamoja na wavumbuvi na watafiti, ukizingatia kua Iraq ina watu wengi wenye vipaji wanaohitaji kusaidiwa kuonyesha vipaji vyao na kuvijali ili visije kuibuliwa na watu wa mataifa mengine na kuelemea huko”.

Mhandisi Jafari Saidi Khayatwi mjumbe wa kamati inayo simamia kongamano na maonyesho hayo akaongeza kua: “Hili ni miongoni mwa makongamano muhimu yanayo fadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, maandalizi yanaendelea kwa kufanya vikao na kujadili mambo ya lazima yatakayo fanyika katika kongamano na maonyesho hayo, Ataba tukufu imeweka kipaombele katika ubunifu wa kisasa utakao saidia maendeleo ya taifa, hivyo kutakua na ubunifu wa kihandisi, kilimo, viwanda, mazingira na tiba”.

Kumbuka kua kongamano na maonyesho yanakusudia mambo yafuatayo:

Kwanza: Kusaidia na kushajihisha akili za wairaq katika uvumbuzi na kuendeleza vipaji.

Pili: Kuchangia katika kufanya tafiti na kuzitafsiri kwa vitendo na kuonyesha mafanikio ya kielimu yanayo changia maendeleo ya taifa kwa wakati mfupi au mrefu.

Tatu: Kunufaika na uvumbuzi hasa wa viwanda na kuchangia pato la taifa.

Nne: Kuchangia katika kuboresha uchumi wa Iraq kupitia wabunifu na watu wenye vipaji vya kubuni miradi.

Tano: Kusaidia wabunifu na watafiti walio fanya vizuri katika hatua ya kutenda walicho kifanyia utafiti au kukigundua.

Sita: Kunufaika na ubunifu wa kiviwanda na kuuingiza katika soko la teknolojia.

Saba: Kujenga uwelewa kwa wananchi wa Iraq kuhusu umuhimu wa wabunifu pamoja na wanavyo gundua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: