Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza tarehe ya kufanyika kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya tano

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza tarehe ya kufanyika kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya tano, litakalo fanywa kwa kushirikiana na kitengo cha Dini chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) ni hazina ya elimu na kilele cha upole), tarehe mosi Rajabu 1440h, sawa na tarehe (9 Machi 2019m).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Aqiil Abdulhussein Yasiriy amesema kua: “Kamati kuu ya maandalizi pamoja na kamati ndogo ndogo zilifanya vikao vingi pembezoni mwa kongamano lililo pita, kwa ajili ya kuweka mikakati ya kongamano hili, ambalo inafaa liendane na utukufu wa muhusika wake”.

Akaongeza kua: “Hakika lengo la kufanya kongamano hili ni kufikisha ujumbe kwa kila mfuasi wa Ahlulbait (a.s), ili aweze kuitambua hadhi ya Imamu Baaqir (a.s) katika kupambana na harakati za waovu na kuzizuwia katika zama zake”.

Yasiriy akasema kua: “Kongamano litakua la siku moja na litakua na vipengele vingi pamoja na kaswida na mashairi, vikiwepo vikao vya mada za kitafiti za hauza na sekula”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) linaangazia nafasi ya pekee aliyo kua nayo, na kuangalia misingi ya kimalezi na kibinaadamu aliyo ifundisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: