Kamati maalumu ya habari katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano yafanya mkutano wa kwanza

Maoni katika picha
Kamati maalumu ya habari katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano imefanya mkutano wa kwanza na kuhudhuriwa na rais wa kamati ya hiyo Ustadh Aqiil Abdulhussein Yasiri pamoja na jopo la wanahabari wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kujadili namna ya kuongeza mawasiliano na vyombo vyote vya habari pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, kwa ajili ya kufikisha mbali zaidi ujumbe wa kongamano.

Rais wa kamati maalumu ya habari katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano Ustadh Aqiil Abdulhussein Yasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika kikao hiki tumeweka mikakati ya utangazaji wa kongamano hili ndani ya siku litakazo fanyika, kwa kutumia luninga, magazeti, redio pamoja na mitandao ya kijamii kwenye intanet”.

Akaongeza kua: “Miongoni mwa mambo yaliyo jadiliwa na kikao hicho ni kutangaza mashindano yatakayo fanyika katika kongamano, ambapo kutakua na shindano la kitabu bora kuhusu Hussein (a.s) pamoja na mashindano ya kaswida za husseiniyya na shindano la mada za kitafiti, hadi sasa tuna idadi ya kutosha ya washiriki, tunasubiri muda wa kupokea kazi za mashindano uishe tuzikabidhi kwenye kamati ya wataalamu kwa ajili ya mchujo”.

Akaendelea kusema: “Tumeweka matangazo maalumu ya kongamano hili katika mji mtukufu wa Karbala, na tumesha andaa mialiko yote ya wageni waalikwa wa kongamano, pia tumesha wasiliana na vyombo vya habari kuhusu kuripoti matukio ya kongamano, tutaweka wepesi wa kushiriki kwa kila anayetaka kuripoti kongamano hili Insha Allah”.

Akasema kua: “Tumekamilisha kuandika kitabu kinacho elezea kongamano la awamu ya kumi na nne, lililo fanyika mwaka jana, tutavigawa kwa wageni wote watakaokuja pamoja na kwenye maktaba na kila mdau wa kongamano”.

Mjumbe wa kamati maalumu ya habari katika kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano Ustadh Hussein Ni’mah amesema kua: “Kikao hiki kimetoka na mapendekezo kadhaa ambayo tutaendelea kuyajadili katika vikao vijavyo, tunatarajia kuongeza wigo wa nafasi za wageni watakao shiriki katika kongamano hili, na ujumbe utakao tolewa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu kama inavyo fanyika kila mwaka”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada husimamiwa na kufadhiliwa kwa ukamilifu na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu kuanzishwa kwake, nalo hufanywa kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), litafanyika mwanzoni wa mwezi wa Shabani ujao –Insha Allah- chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein –a.s- ni mnara wa umma na suluhisho la misingi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: