Kwa mara ya kwanza hapa Iraq: Hospitali ya rufaa Alkafeel yafanya matibabu makubwa bila kusaidiwa na wataalamu wa nje…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mkakati wake wa kufikia uwezo wa kutoa matibabu kwa kiwango cha juu kabisa, Hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanya matibabu ya kisasa ambayo yanafanyika hapa Iraq kwa mara ya kwanza, matibabu ya kutumia mionzi bila kufanya ubasuaji ambao unaweza kutela matatizo kwa mgonjwa, matibabu ya kutumia mionzi yapo chini ya idara maalumu ndani ya hospitali inayo itwa idara ya matibabu kwa kutumia mionzi.

Kwa mujibu wa maelezo ya uongozi wa hospitali idara hiyo inafanya kazi chini ya jopo la madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya Iraq, jopo hilo linaongozwa na Dokta Adnani Zubaidi daktari bingwa wa mionzi, aina ya wagonjwa wanao pokelewa na idara hii ni:

  • 1- Vimelea vibaya, miongoni mwa aina za vimelea ni: (vimelea kwenye fiko, vimelea kwenye kibofu cha mkojo, vimelea kwenye ini, vimelea kwenye njia ya mkojo na sehemu zinginezo).
  • 2- Vimelea vizuri, miongoni mwa vimelea hivyo: (vinahusisha kibofu cha mkojo na nyumba ya uzazi na hutibiwa kwa kupandikiza vijiti).
  • 3- Vijiti hupandikizwa kabla ya hatua ya upasuaji, katika magonjwa yafuatayo:
  • Vimelea vya fiko na ini.
  • Vimelea kwenye korodani.
  • Viimelea kwenye macho sawa tatizo liwe kwenye ubongo au mshipa wa fahamu na vinginevyo.
  • Vimelea vya kwenye miguu.
  • Vimelea vya kwenye ubongo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili jioni kwenye namba zifuatazo: (07602329999 / 07602344444 / 077306222230).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: