Mradi wa vikao mjadala wahitimisha awamu ya kwanza na wajiandaa na hatua inayo fuata…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha Dini idara ya tabligh imehitimisha sehemu ya kwanza ya mradi wa vikao mjadala kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq, vimeshiriki vyuo vikuu mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, mradi huu unalenga kutoa malezi bora kwa wanafunzi wakiume na wakike, na kuwajengea uwezo wa kupambana na changamoto za maadili mabaya na vita ya kifikra.

Mkuu wa mradi huu ambaye ni kiongozi wa idara ya tabligh Sayyid Muhammad Mussawi amesema kua: “Vikao mjadala vinalenga kuongeza kiwango cha uwelewa kifikra na kitamaduni kwa wanafunzi, tunatarajia kua na matokea chanya katika familia na jamii, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tunasikilizwa na kufatiliwa vizuri na wanafunzi, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) tumemaliza sehemu ya kwanza ya mradi wa vikao mjadala kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, mradi huu umeanza mwanzoni mwa mwaka huu wa masomo, vikao hivi vinampa kila mtu haki ya kuzungumza, lengo lake ni kuwafundisha wanafunzi nafasi tukufu aliyo nayo mwanaadamu na nafasi ya mwanafunzi, na umuhimu wake katika kujenga jamii, pamoja na kutilia msisitizo mambo ya kimaadili na kimalezi”.

Akaongeza kua: “Tumekamilisha maandalizi ya msimu wa pili kwa utaratibu uleule, tunahusisha vyuo vingi zaidi ili wanafunzi wengi wanufaike na ratiba hii, kwa kufuata ratiba iliyo pangwa, inayo endana na umri wa wanafunzi na inayo jibu mahitaji yao, ratiba inatekelezwa kwa kuwasiliana na kushirikiana na wakuu wa vyuo na maahadi, pia ratiba hii inavipengele vingi, kuna kipengele cha wakufunzi na kipengele cha wanafunzi wa vyuo, kipengele cha vikao mjadala ni moja kati ya vipengele vingi vinavyo simamiwa na Ataba tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: