Idara ya shule za Alkafeel za wasichana imemaliza ratiba ya hema la Skaut kwa wanafunzi wa vyuo

Maoni katika picha
Hivi karibuni idara ya shule za wasichana za Alkafeel ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imemaliza ratiba ya hema la Skaut la msimu wa likizo za majira ya baridi lililo pewa jina la (Mabinti wa Abida/ mafunzo ya Riyahaini ya Ikhlasi), lililo andaliwa rasmi kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaosoma vyuo vikuu, wameshiriki kutoka mikoa tofauti (Bagdad, Najafu, Karbala, Waasit na Dhiqaar), ratiba hii imeandaliwa kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo za majira ya baridi kwa manufaa ya wanafunzi, na inasaidia kuwajenga kiutamaduni.

Hema liliwekwa katika uwanja wa kituo cha Swidiqah (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lilikua na vipengele vingi kutokana na ratiba iliyo pangwa, Ustadhat Bushra Alkinani mkuu wa idara ya shule za Alkafeel za wasichana ameongea kuhusu ratiba ya hema hilo kuwa: “Idara yetu chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikifanya harakati mbalimbali za wasichana katika kipindi cha mwaka mzima, pamoja na kuweka umuhimu zaidi katika vipindi vya likizo za majira ya joto na baridi, hema hili ni sehemu tu ya harakati nyingi tunazo fanya, katika hema hili kulikua na vipengele vingi, vinavyo endana na mahitaji ya tabaka hili, miongoni mwa vipengele vilivyo kuwepo katika ratiba ni:

  • - Mihadhara ya Fiqhi na Aqida pamoja na kutoa nafasi ya majadiliano.
  • - Mihadhara ya maendeleo ya kibinaadamu.
  • - Mihadhara ya kimatibabu na namna ya kujikinga na maradhi tofauti.
  • - Kuwapa nafasi ya kuongea kwa ajili ya kubaini vipaji na uwezo wao.
  • - Mihadhara ya namna ya kupambana na changamoto ya vyombo vya habari visivyo faa.
  • - Kufanya mashindano ya vikundi.
  • - Kutembelea maeneo mbalimbali ya Atabatu Abbasiyya tukufu na vitengo vyake vya kisekula.
  • - Kufanya matukio mbalimbali.

Kumbuka kua hema ni moja ya harakati za idara ya shule za Alkafeel za Qur’ani na hufanyiwa katika kituo cha Swidiqah (a.s), kusudio la mradi huu ni kufanya jambo endelevu kwa wanafunzi katika kipindi cha mwaka mzima, kwa namna ambayo wataweza kupewa mada za kielimu za masomo tofauti yenye umuhimu kwao, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao na kukuza vipaji pamoja na kuwajenga kijamii, hivyo hupewa mihadhara mbalimbali inayo wataka wawe makini na wajitahidi kutatua changamoto za jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: