Mazingira ya kipindi cha likizo katika malalo mawili matukufu na eneo la katikati yake

Maoni katika picha
Kama kawaida yake katika vipindi vya likizo na siku za mapumziko, familia za wairaq ziishizo ndani na nje ya mkoa wa Karbala huenda kutembelea malalo takatifu kwenye miji tofauti, na malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) hutembelewa na watu wengi zaidi, familia huondoka pamoja na watoto wao kwa ajili ya kuja kufanya ziara maalumu, wakitumia vizuri fursa ya likizo, humaliza muda wao wakiwa pembeni ya maeneo hayo matakatifu.

Mji huu mtukufu umeshuhudia maelfu ya mazuwaru waliokuja kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq, na wengine wakitoka nje ya Iraq, wanakuja kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na uwanja wa katikati ya haram mbili umefurika mazuwaru, muda wote harakati zao hazipungui na hasa siku ya Alkhamisi na Ijumaa.

Atabatu Abbasiyya tukufu inatumia wingi wa mazuwaru hao kutangaza baadhi ya maelekezo ya Dini na kimaadili kwa kutumia vipaza sauti vilivyo wekwa katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kama sehemu ya kumzawadia zaairu mambo yenye manufaa kwake duniani na akhera, pia kuna mihadhara ya kidini ambayo hutolewa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) au nje, mada mbalimbali huzungumzwa katika mihadhara hiyo, pamoja na kufungua mlango wa kuruhusu maswali kutoka kwa mazuwaru muda wote, yote hayo ni kwa ajili ya kuhakikisha zaairu mtukufu ananufaika na ziara yake kwa kiasi atakavyo weza.

Mambo hayaishii hapo, vitengo vya utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu vimeandaa sehemu za malazi na kuweka vifaa vya kulalia na kujifunika, ili kumuwezesha zaairu anayetaka kulala na kupumzika aweze kulala kwa amani na utulivu, hali kadhalika zimeandaliwa sehemu za kuswali swala za jamaa, pia Atanatu Abbasiyya imeamua kusimamisha kazi zote za ukarabati ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi (a.s), kwa ajili ya kutoathiri harakati za mazuwaru na utekelezaji wa ziara, pia tumerahisisha uingiaji na utokaji ndani ya haram tukufu kwa wanaume na wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: