Mada za kongamano:
- - Mbinu za kutunza elimu ya makumbusho.
- - Makumbusho katika mtazamo wa elimu na mawasiliano ya kijamii.
- - Mbinu za kisasa katika maonyesho ya makumbusho.
- - Elimu na mbinu mpya katika kulinda majengo ya makumbusho.
- - Mbinu za kielimu na vifaa vipya katika kusanifu makumbusho zinazo tembelewa na zisizo tembelewa.
- - Kujenga uwezo wa watumishi wa makumbusho.
Masharti ya kushiriki:
- 1- Utafiti uhusu moja ya mada tulizo taja.
- 2- Mtafiti azingatie vigezo vya kielimu vinavyo kubalika kimataifa, na aandike kwa moja ya lugha mbili (kiarabu au kiingereza).
- 3- Utafiti uandikwe kwenye karatasi ya (A4) na auhifadhi katika (CD) na uwe na kurasa 15 hadi 30, uandikwe kwa hati ya (Simplified Arabic) na ukubwa wa maandishi uwe saizi (14) na atautuma kwa njia ya barua pepe ya kongamano.
- 4- Usiwe umesha wahi kusambazwa kabla au kushiriki kwenye kongamano au nadwa.
- 5- Utumwe muhtasari wa utafiti kwa moja ya lugha mbili, kiarabu au kiengereza, na usizidi maneno (300) pamoja na wasifu (cv) ya mwandishi.
- 6- Mwisho wa kupokea mihtasari ya tafiti ni (1/ 5/ 2019m).
- 7- Mwisho wa kupokea tafiti kamili ni (1/ 8/ 2019m).
- 8- Tafiti zitaingizwa katika mchujo wa kielimu ili kupata zitakazo shiriki kwenye kongamano.
- 9- Kamati inayo simamia kongamano itawajibika kuwagharamia watafiti kipindi chote cha kongamano.
- 10- Mtafiti atakaye kubaliwa aandike utafiti wake kwenye (PowerPoint) maalumu.
- 11- Tafiti zitumwe kwenye barua pepe zifuatazo: musema@gmail.com au musem@alkafeel.net kwa maelezo zaidi piga moja na namba za simu zifuatazo (009647802618476 / 009647702728492 / 009647709721010).
Kumbuka kua kongamano linalenga:
- - Kutoa wito wa kulinda urithi na mazingira.
- - Kusaidia taasisi za kidini na kijamii kuendeleza mazingira.
- - Kufungua milango ya kusaidiana kwa taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa.
- - Kuinua kiwango cha utendaji wa makumbusho na kuboresha idara zake.