Mkakati wa kushirikiana kati ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na wilaya ya Samara katika kuomboleza kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s).

Maoni katika picha
Mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Ustadh Maitham Zaidi katika ziara yake kwenye mkoa wa Swalahu Dini na baada ya kukutana na kaimu mkuu wa wilaya ya Samara Ustadh Mahmudu Khalf Ahmadi, ametangaza ushirikiano na mkakati wa kuimarisha ulinzi na kuboresha utowaji wa huduma katika kuhuisha ziara ya kukumhuka kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s) katika mwezi wa Rajabu Aswabu.

Mushrifu ameviambia vyombo vya habari kua: “Nimefanya ziara hii baada ya mawasiliano yaliyo lenga kuunganisha juhudi na kuweka mkakati kamili wa swala hili, kushiriki Atabatu Abbasiyya tukufu katika kutoa huduma na mambo ya kihandisi pamoja na kusafisha sehemu itakayo kua maegesho ya magari yatakayo leta mazuwaru watukufu katika mji wa Samara”. Akathibitisha utayali wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wa kulinda amani kwa ajili ya kufanikisha ziara pamoja na kikosi cha ulinzi wa Samara.

Naye kaimu mkuu wa wilaya ya Samara Ustadh Mahmudu Khalf Ahmadi amekishukuru kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji pamoja na mushrifu (kiongozi mkuu) wake kwa kuijali Iraq pamoja na mji wa Samara kwa namna ya pekee kabisa, akatoa wito kwa vikosi vingine vifuate nyayo za kikosi cha Abbasi (a.s) katika kuimarisha undugu na kushikamana pamoja kwa ajili ya Iraq moja, sambamba na kufelisha njama zote za kutengana zinazo chochewa na magaidi.



Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: