Program ya Saai Al-Ameed inatumia vizuri muda katika utendaji wa kazi za kiofisi

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutumia program ya (Saai Al-Ameed) ambayo ni program maalumu ya kuunganisha kielekronik kazi za kiofisi zinazo fanywa na taasisi za kielimu za Al-Ameed, pamoja na kamati ya malezi na elimu ya juu, na wakuu wa vitengo. Asubuhi ya Jumamosi ya tarehe (10 Jamadal Thani 1440h) sawa na tarehe (16/02/2019m) imekamilika program hiyo, na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Dida na baadhi ya watumishi kwa ajili ya kufanya warsha ya kuitambulisha na kuitangaza rasmi pamoja na kuanza kuitumia.

Mtengenezaji wa program hiyo katika kitengo cha malezi na elimu ya juu, Ustadh Muhammad Tamimi amesema kua: Program ya Saai Al-Ameed ni program bora ya kutuma na kupokea ujumbe katika kitengo cha malezi na elimu ya juu, pamoja na kamati ya malezi na elimu ya juu, inaunganisha shule za awali, za msingi, maahadi na vyuo vikuu katika idara ya kitengo na kamati yake.

Akaongeza kusema kua: Unaweza kutuma na kupokea ujumbe kwa wakati mmoja, na unaweza kuchapisha vitabu na kuvihifadhi kielektronik, pamoja na faharasi ya kielektronik; inayo rahisisha kuwasili vitabu kwa haraka na kuweka maelezo maalumu au kuambatanisha na barua, unaweza kupata maelezo yote.

Ustadh Mustwafa Hakim muhudumu wa program ya Saai Al-Ameed, amesema kua: Tumeandaa vifaa vyote vinavyo hitajika kama vile kompyuta, printa na mashine za kupiga fotokopi (kurudufu) pamoja na kuweka huduma ya Intanet, na program wezeshi ya Saai Al-Ameed, tuna mawasiliano ya moja kwa moja na vituo vyote kwa ajili ya kutatua tatizo lolote linalo weza kujitokeza.

Kama alivyosema kiongozi wa idara katika kamati kuu Ustadh Yusufu Kabah: program ya Saai Al-Ameed imetusaidia kuokoa muda, tunaweza kutuma ujumbe kwa haraka na kuuhifadhi kwa uhakika, faharasi yake ipo kielektronik, inarahisisha kuwasili barua katika dakika ileile unayo ituma, tofauti na kutumia karatasi na wino.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: