Kuhitimisha semina ya kuandaa wasomaji wa Iraq…

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuisha kwa semina ya kujenga uwezo iliyo fanyika ndani ya mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji wa Iraq awamu ya nne katika kipindi cha likizo.

Wanafunzi walioshiriki wamefanyiwa mtihani wa majaribio mbele ya kamati ya wataalmu walio simamia semina, wanafunzi (11) wamefaulu kuingia katika kozi ya kwanza, wataungana na wenzao waliochaguliwa kusoma kozi hiyo, kamati ya wataalamu waliosimamia semina ndio walioamua hivyo kutokana na uwezo ulio onyeshwa na wanafunzi hao wakati wa semina.

Kumbuka kua mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji wa Iraq ni moja ya miradi mikubwa inayo endeshwa na kituo cha miradi ya Qur’ani cha Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tangu mwaka (2013) unalenga kuandaa wasomaji wazuri wa Qur’ani, kwa ngazi tofauti, kuna ngazi ya kwanza na ya pili, muhimu zaidi ni semina za (Tamhidi, kuandaa, kujenga uwezo, kozi na takhasusi…) kwa ufupi ni program kamili yenye vipengele vingi sambamba na kushirikiana na wasomaji wa Qur’ani mahiri kutoka Misri, tunapewa ushirikiano mzuri na watu wa Misri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: