Skaut ya Alkafeel imemaliza mafunzo ya Skaut awamu ya tatu…

Maoni katika picha
Hivi karibuni jumuiya wa Skaut ya Alkafeel ambayo ipo chini ya idara ya watoto na makuzi katika Ayabatu Abbasiyya tukufu imemaliza mafunzo ya Skaut awamu ya tatu, yaliyo pewa jina la (Rabiu Ma’arifah) chini ya anuani ya (Hema la Zaharaa –a.s-), katika mafunzo hayo wameshiriki zaidi ya wanafunzi (600) ambao ni wanachama wa Skaut wenye umri kati ya miaka (10 – 18) waliopo katika Skaut za (Alshabaal, Alkashaafah na Aljawaalah) kutoka katika shule zote za serikali zilizopo katika mji wa Karbala pamoja na kwenye jumuiya zingine za Skaut kutoka mkoa wa Baabil na Basra.

Hafla ya kufunga imefanyika ndani ya ukumbi mkuu uliopo katika jengo la Shekh Kulaini (q.s) ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na washiriki pamoja na wazazi wao bila kusahau viongozi mbalimbali, baada ya kusomwa Qur’ani ya ufunguzi na surat Fatiha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na kuimba wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya, ulifuata ujumbe kutoka katika idara ya watoto na makuzi ulio wasilishwa na kiongozi wa idara hiyo Ustadh Sarmad Saalim, miongoni mwa aliyosema ni: “Miongoni mwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutokana na ukarimu na utukufu wake, na kwa utukufu wa raudha yake takasifu, tumepata moyo wa kufanya kazi na vijana wameonyesha utayali wa kufuata mwenendo wa waja wema miongoni mwa watu wa kizazi cha Mutume (s.a.w.w), tunatarajia kuona mradi huu unatengeneza watu wenye lengo la kumridhisha Mwenyezi Mungu mtukufu na kuwafuata wale ambao ni kigezo chema miongoni mwa Manabii, Maswidiqiin, Mashuhadaa na hao ndio marafiki wema”.

Akaoneza kua: “Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ni moja ya idara za watoto na makuzi ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga watoto na vijana waliopo katika shule za msingi na sekondari, inawapa malezi mema kwa kufuata misingi na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa kutumia ratiba maalumu kwa ajili hiyo, wanafundishwa maadili mema na itikadi sahihi, na kuwafanya waweze kutumia uwezo wao wa kibinaadamu na kiubunifu pamoja na kuwafungamanisha na kiigizo chema katika Dini, ambacho ni mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s)”.

Saalim akaendelea kusema kua: “Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inatoa mafunzo mbalimbali, yakiwemo mafunzo haya ya Rabiu Maarifah ambayo yamefanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo, yamehusisha uwekaji wa mahema yaliyo pewa jina la bibi Zaharaa (a.s), wameshiriki watoto wengi kutoka mkoa wa Karbala na Baabil”.

Kisha ukafuata ujumbe wa Skaut ya Alkafeel ulio wasilishwa na mkuu wa mipango na mafunzo Dokta Zamani Kinani, akasema kua: “Hakika ratiba ya Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ni ya kibinaadamu na kimaadili, inatekeleza jukumu la kitaifa na kidini, Jumuiya inatarajia kujenga vijana wenye uwelewa, waumini na wanao shikamana na misingi ya kibinaadamu, wenye uzalendo wa taifa lao na upendo wa jamii zao wanaoweza kujenga vizuri taifa hili”.

Akaongeza kua: “Kupitia uhakiki na kufanya program mbaalimbali za kila wiki, kila msimu na kila mwaka, ikiwa ni pamoja na program za kuongeza uwezo kwa ujumla, Rabiu Maarifah na program ya Skaut ya malezi ya kielimu, tunataka kijana atumie vizuri wakati wake wa likizo, tuweze kuibua vipaji na kukuza uwezo wa akili pamoja na kuendelea kulea vitu hivyo chini ya wataalamu walio bobea katika mambo ya Dini na sekula pamoja na wakufunzi wa maendeleo ya kibinaadamu”.

Ujumbe wa shule zilizo shiriki uliwasilishwa kwa niaba yao na Ustadh Hashim Jawadi Ali, ameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na viongozi wake pamoja na idara za shule zilizo shiriki katika hema hizi, akasisitiza kua Jumuiya imepata mafanikio makubwa kutokana na hii program, tunatarajia kuona inapanua wigo zaidi siku za mbele, hafla imepambwa na maigizo pamoja na filamu inayo onyesha baadhi ya mambo yaliyo fanyika katika program ya Skaut (Rabiu Ma’arifah), mwisho kabisa washiriki wakapewa vyeti vya ushiriki pamoja na wale walio changia kufanikiwa kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: