Vinasikika visomo vizuri vya Qur’ani ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka mazinira bora ya kiroho…

Maoni katika picha
Kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w): (Kila kitu kina pambo na pambo la Qur’ani ni sauti nzuri), na kufuatia harakati za Qur’ani zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’ani chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefanyika mahafali ya Qur’ani ambyo ni miongoni mwa mahafali za mradi wa Arshu Tilawa wa kila waiki.

Katika mahafali hii wameshiriki wasomaji mahiri walio toa ushindani kwa wasomaji wakubwa wa Qur’ani, wasomaji hao ni Muhammad Jaasim Swabru, mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji, na msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhammad Ridhwa Salmani, na kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran alisoma Ustadh Ahmadi Abu Qassimy mmoja wa wakufunzi wa kozi ya mradi wa kuandaa wasomaji wa Iraq.

Mazuwaru watukufu pia wameshiriki katika mahafali hiyo, walizunguka jukwaa kuu na kutafakari aya za kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, wakisikiliza sauti za wasomaji mahiri ndani ya jengo hilo takatifu, sambamba na wale waliokua wakifuatilia moja kwa moja kupitia luninga ya Karbala.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya inaendesha miradi mingi ya Qur’ani, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, nao unalenga kunufaika na uwezo walionao watoto katika usomaji wa Qur’ani na kuutangaza katika ulimwengu wa kiislamu, na kufanya kazi ya kuvilea na kuviendeleza vibaji hivyo kwa kufuata utaratibu maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: