Atabatu Abbasiyya tukufu imepata moja ya tuzo kubwa katika mashindano ya kitabu cha hauza cha mwaka…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imepata nafasi ya pili katika shindano la kuandika kitabu cha masomo ya hauza ya kwaka mmoja, shindano hili linafanyika kwa mara ya ishirini katika mji mtukufu wa Qum, kupitia tolea la kitabu walicho hakiki cha (Qit’atun min kitaabil futuuhi) kilicho andikwa na Ibun A’tham Kufiy aliye fariki mwaka 320h, nacho ni mingoni mwa vitabu vilivyo hakikiwa na shekh Qais Atwaar (d.t) na kua miongoni mwa matoleo ya kituo cha kuhuisha turathi kilicho chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Makumi ya vitabu vya turathi vilivyo fanyiwa uhakiki katika nchi tofauti za kiislamu na kiarabu yameshiriki katika shindano hili kupitia taasisi na maktaba zao, kitabu hiki kimepata nafasi ya pili, mafanikio haya ni muendelezo wa mafanikio ya aina hii yaliyo patikana katika mashindano yaliyo pita.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilipata tuzo ya juu katika mashindano kama haya ya kuhakiki, kutunga na kusambaza yaliyo fanyika mwaka jana, kituo cha kuhuisha turathi kilipata nafasi mbili za juu, nafasi ya kwanza na ya pili kupitia vitabu vyake: Mausua ya Alammah Urdubadi (nafasi ya kwanza) na kitabu muhtasar katika habari mashuhuri na Maimamu kumi na mbili cha Ibun Twaqtwaqi (nafasi ya pili).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: