Sayyid Alaa Mussawi Rais wa wakfu Shia amepongeza ushiriki wa Atabatu Abbasiyya katika kutangaza mafundisho ya Dini ya kiislamu na kulinda misingi sahihi ya kiislamu na kuendana na maendeleo ya kielimu na kitamaduni, na akapongeza ushiriki wake endelevu katika maonyesho haya.
Aliyasema hayo baada ya kutembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Bagdad, na kuangalia vitabu vinavyo onyeshwa na Ataba tukufu, pamoja na kusikiliza maelezo kuhusu bidhaa zinazo onyeshwa na tawi hilo ambalo limewakilishwa na kitengo cha elimu na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.
Mheshimiwa Mussawi alisema kua: “Nimefarijika sana kutembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu na kuona aina nzuri za vitabu ambavyo ni kielelezo cha mafanikio, namuomba Mwenyezi Mungu abariki juhudi hizi za kielimu na kiutamaduni na awape nguvu ya kuendelea kuitumikia elimu na watu”.
Kumbuka kua tawi la Atabatu Abbasiyya limejaa machapisho ambayo ni vitabu tofauti vya Dini na mambo mengine, pia kuna maonyesho ya mtandao wake wa kielektronik (Mtandao wa kimataifa Alkafeel) ulioanzishwa na wataalamu wa Ataba, vilevile wanaonyesha kazi iliyo fanywa na Ataba ya kuanzisha mtandao wa kielektronik wenye vitabu vya kisekula ambao ni msaada mkubwa kwa wanafunzi na watafiti, maktaba hiyo inamaelfu ya vitabu vya masomo mbalimbali ya elimu ya juu, hali kadhalika Atabatu Abbasiyya tukufu hushiriki mara nyingi katika maonyesho na makongamano ndani na nje ya Iraq, matawi yake hupata mwitikio mkubwa, na huwa na ongezeko la vitabu vipya katika kila maonyesho.