Kamazi za maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada zinaendelea na vikao vyake…

Maoni katika picha
Kamati za maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano zinaendelea kufanya vikao vyake, kwa ajili ya kuangalia mahitaji yao kwa namna ambayo zitafanikisha kufanyika kongamano zuri kama yaliyo pita, na linalo endana na utukufu wa tukio husika, idadi ya vikao inaongezeka kadri muda wa kongamano unavyo karibia, nalo litafanyika mwanzoni mwa mwezi wa Shabani chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni mnara wa umma na suluhisho madhubuti).

Miongoni mwa mambo yaliyo jadiliwa katika kikao cha mwisho ni namna ya kuteua na kualika watu, mjimbe wa kamati ya maandalizi Sayyid Adnani Mussawi amesema kua: “Kikao hiki ni mwendelezo wa vikao vilivyo pita na tumejadili kuhusu watu watakao shiriki katika kongamano, kamati imependekeza kuchagua watu wengi zaidi ya (90) watakao kuja kushiriki katika kongamano, wakiwa ni waandishi na watafiti wa hauza au sekula kutoka ndani na nje ya Iraq”.

Pia kamati imependekeza kuongeza vipengele vingine katika kongamano la mwaka huu, vitakavyo liwezesha kufukia malengo yake, mjumbe wa kamati ya maandalizi Ustadh Ali Kaadhim Sultani akasema kua: Kuna vipengele viwili vipya vitakavyo fanyika mwaka huu, navyo ni shindano la kuandika kitabu kuhusu Imamu Hussein (a.s) na shindano la mashairi, vipengele hivyo vimesha pata idadi nzuri ya washiriki”.

Maniyyuna akafafanua kua; kuongeza vipengele katika kongamano la mwaka huu kunazidi kuonyesha umuhimu wa kongamano hili na malengo yake ni hatua kubwa na nzuri inayo onyesha uboreshaji wa kongamano kutoka hatua fulani hadi hatua nyingine.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada huandaliwa na kusimamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad Zainul-Aabidina (a.s), ni moja ya harakati inayofanywa na Ataba mbili tukufu kwa pamoja kila mwaka, na zinalichukulia kua sehemu ya kuelimisha umma kidini na kifikra, pamoja na kubainisha athari na matokeo ya mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s), kongamano la awamu ya kumi na nne lilihudhuriwa na watu kutoka nchi (33) duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: