Kumbukumbu ya kifo cha Ummul Banina (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya maombolezo na mazingira yake yamejaa huzuni…

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na kukumbuka kifo cha Ummul Banina (a.s), korido zake zimewekwa mapambo meusi na kuta zimefunikwa vitambaa vyenye ujumbe unao ashiria huzuni, hakika msiba huu unaumiza sana nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Kama kawaida ya kuomboleza vifo vya Ahlulbait (a.s) Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya uombolezaji na utumishi katika tukio hili linalo umiza roho ya kila muumini, ratiba inamambo yafuatayo:

  • - Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kimejipanga kupokea mawakibu za waombolezaji zitakazo kuja kutoka ndani na nje ya Karbala tukufu kumpa pole Abulfadhil Abbasi (a.s), ikizingatia kua yeye ndio muhusika mkuu wa msiba huu, mawakibu hizo zitaingia katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya siku mbili zijazo.
  • - Kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram tukufu ya Abbasi siku ya Jumapili na Jumatatu, mzungumzaji wa majlisi hizo atakua ni shekh Abdullahi Dujaili na itafuata matam kutoka kwa bwana Baasim Karbalai.
  • - Kitengo cha Dini cha Atbatu Abbasiyya kitatoa mihadhara kadhaa ya kidini ndani ya ukumbi wa haram tukufu, pamoja na mihadhara maalumu kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika majlisi zitakazo fanywa ndani ya ukumbi wa utawala.
  • - Kama kawaida katika kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya watafanya matembezi ya pamoja kwenda kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Idhaa ya Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa vipindi maalumu vya kumzungumzia Ummul Banina (a.s) na nafasi ya pekee aliyo nayo kwa wanawake wa kiislamu.
  • - Mtandao wa kimataifa Alkafeel –mtandao rasmi wa Ataba- utafawafanyia ziara mbele ya kaburi lake tukufu huko Baqii watu woto watakao jisajili katika ukurasa wake wa ziara kwa niaba.
  • - Mgahawa (Mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) utaandaa maelfu ya sahani za chakula na kugawa bure kwa mazuwaru kufuatia tukio hili.
  • - Vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu vimekamilisha maandalizi ya kuwapokea mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) watakao wasili ndani ya siku mbili zijazo, vimejiandaa kuhakikisha mazuwaru wanafanya ibada kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: