Tumia fursa hii kumzuru Ummul Banina (a.s) katika kaburi lake tukufu…

Maoni katika picha
Miongoni mwa utaratibu wake wa kuwasiliana na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na kudumisha uhusiano baina yao na maimamu wao (a.s), mtandao wa kimataifa Alkafeel kupitia ukurasa wa ziara kwa niaba itafanya ibada ya ziara na kusoma dua kwenye kaburi tukufu la Ummul Banina (a.s) huko Baqii katia mji wa Madina, kufuatia kumbukumbu ya kifo chake, unaweza kujisajili kupitia anuani hii: https://alkafeel.net/zyara/ .

Utafanyiwa ziara na waumini waliojitolea kutumikia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na wenye mapenzi makubwa kwa Ummul Banina (a.s), watafanya ziara hiyo na zinginezo pamoja na kuswali rakaa mbili kwa kila anayetaka kufanyiwa hivyo kutoka kila kona ya dunia.

Tunapenda kufahamisha kua mtandao wa kimataifa Alkafeel unaukurasa maalumu wa ziara kwa niaba katika kila toghuti miongoni mwa toghuti zake na kwa lugha zote zilizopo katika mtandao wetu, ukurasa huu ni maalumu kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka kila sehemu ya dunia, ambao hawawezi kuja kufanya ziara wao wenyewe moja kwa moja hapa Iraq au nchi zingine, hii ni fursa nzuri ya kufanya ziara kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu mwingine unayetaka afanyiwe ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: