Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya maombolezo ya kifo cha Ummul Banina (a.s)…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul Banina (a.s), ndani ya haram tukufu ya mtoto wake Abulfadhil Abbasi (a.s), majlisi hizo zitadumu kwa muda wa siku mbili chini ya uhadhiri wa Shekh Abdullahi Dujaili na mwimbaji mkongwe Baasim Karbalai na kuhudhuriwa na watu wengi miongoni mwa waombolezaji na mazuwaru wa malalo ya mwezi wa familia (a.s).

Majlisi hizi ni sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu isemayo: (Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo), kuhuisha kifo cha Ummul Banina (a.s) na maasumina wengine (a.s) pamoja na watu wa familia zao ni jambo muhimu, waumini wanatakiwa kufanya hivyo na kuhimiza jambo hilo, kwani matukio haya yanamasomo na mazingatio ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi katika maisha yetu.

Majlisi zinafanywa baada ya swala ya Ishaa, hufunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha hufuatia muhadhara wa Shekh Abdullahi Dujaili, amabye huzungumzia utukufu wa mama huyu matakasifu.

Baada ya muhadhara hufuata matam na nauha ambazo husomwa na Baasim Karbalai, huimba kaswida zinazo zungumzia utukufu wake, subira na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, mama huyu ananafasi kubwa kwa Ahlulbait (a.s), kutokana na jinsi alivyo jitolea watoto wake wanne waende kumnusuru Imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya kulinda Dini ambayo bani Umayya walijaribu kuharibu misingi yake.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya maombolezo yenye vipengele vingi, kuna utowaji wa mihadhara, majaalisi za kuomboleza na imetangaza utayali wake wa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, wanaokuja kumpa pole Imamu Hussein na nduhu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: