Uaminifu kwa nia yake: Mula Baasim Karbalai aipa makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu taji la dhahabu…

Maoni katika picha
Mwimbaji mkongwe wa kaswida za Husseiniyya bwana Baasim Karbalai ametoa taji alilopewa hivi karibuni na wapenzi wake katika mji wa Kadhimiyya na kulikabidhi kwenye makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, taji hilo alipewa kama zawadi kutokana na jinsi anavyo watumikia watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa miaka mingi, akitumia sauti yake nzuri kuimba kaswida na mashairi ya huzuni na furaha pamoja na kuonyesha mapenzi kwa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Bwana Baasim Karbalai amesema kua wanaofaa kupewa taji hili ni watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwa hiyo nimeona nikabidhi taji hili kwa makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wakati wa kukabidhi akasema kua: (Taji linamfaa mlezi wake) akimaanisha Abulfadhil Abbasi (a.s).

Karbalai amebainisha kua: “Hakika watu wa maukibu walinishtukiza kwa kunipa zawadi hii na mimi nikaikubali, lakini ndani ya nafsi yangu kuanzia muda huo nilikusudia kuitoa zawadi hii kwa moja ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya au Abbasiyya, kwenye moja ya makumbusho ya Ataba hizo, naamini kua kila jambo zuri ninalo pata linatokana na wao, na uwepo wangu ni kwa utukufu wao, najuvunia kuoewa taji la kuwa mtumishi wa Husseini”.

Akaongeza kua: “Mwanzoni nilitahayari niikabidhi katika makumbusho ipi, ikabidi nifanye istikhara ya kisheria ndipo nikapata jibu la kuikabidhi katika makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa mambo ya pekee yaliyo jitokeza kukabidhi huku kumesadifu siku ya kifo cha mama yake Abulfadhil Abbasi bibi Fatuma Ummul Banina (a.s)”.

Akamaliza maelezo yake kwa kwa manane yanayo ashiria taji yasemayo: “Taji linamfaa mlezi wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: