Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa na uongozi wa wapa zawadi kuonyesha kujali ushiriki wake…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu imemaliza ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yaliyo fanyika Bagdadi chini ya kauli mbiu isemayo: (kitabu kimoja ni zaidi ya uhai) kuanzia tarehe (7) hadi (18) Februari.

Huu ni mwendelezo wa ushiriki wa miaka ya nyuma, Atabatu Abbasiyya tukufu imekua daima ikishiriki katika maonyesho hayo, katika ushiriki wa mwaka huu kumekua na mwitikio mkubwa sana wa watu waliotembelea maonyesho, hasa wawakilishi na mawakala wa vituo vya usambazaji wa vitabu na maktaba, wamechukua kwa wingi machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pia inatokana na ubora wa machapisho hayo ikizingatia kua yanamada tofauti zilizo andikwa vizuri.

Kamati iliyosimamia maonyesho imelipa zawadi tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu ikiwa kama ishara ya kuthamini ushiriki wake katika maonyesho haya, na kuomba iendelee kushiriki maonyesho mengine yajayo.

Tawi la Ataba lilikua na machapisho mbalimbali yanayo maliza kiu ya wasomaji wa aina zote, mtoto hadi mzee, tena katika sekta tofauti, hawajajibana kwenye sekta moja na kuacha zingine, kila aliye tembelea tawi hilo amesifu machapisho ya Ataba, asilimia kubwa ya viongozi wa kijamii na kisekula wamefurahishwa sana na machapisho ya Ataba tukufu, na wamesema kua Atabatu Abbasiyya tukufu imefanikiwa kuomuonyesha zaairu kua ni taasisi kubwa ya kitamaduni.

Hali kadhalika wasimamizi wa tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu walikua na fursa kubwa ya kuangalia machapisho ya vituo vingine vilivyo shiriki katika maonyesho hayo, kutoka nchi mbalimbali duniani.

Fahamu kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa ambayo hufanywa Bagdad ni sehemu muhimu ambayo Atabatu Abbasiyya huitumia kuwasiliana na watu wa nje, kupitia machapisho ya vitabu vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: