Atabatu Abbasiyya yakusudia kufanya awamu ya saba ya kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s) katika jimbo la Kashmiri…

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kufanya kongamano la kitamaduni la Amirul Mu-uminina (a.s) awamu ya saba katika jimbo la Kashmiri nchini India chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirul Mu-uminina (a.s) ndio njia iliyo nyooka na kamba madhubuti ya Mwenyezi Mungu), katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, tunatarajia kushiriki Ataba zote katika kongamano hilo (Atabatu Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya na Askariyya) pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ndio waandaaji wa kongamano, pia Ayatullahi Yusufu (ambaye ni mwenyeji wa mji huo) atahudhuria, kongamano hilo litafanyika tarehe (13 – 17) Rajabu Al-Aswabu (1440h).

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati ya maandalizi kongamano litakua na vipengele vingi kuhusu hadhi (shakhsiyya) ya Amirul Mu-uminina (a.s) kwa namna ambayo litaendelea kulinda ubora ulio onekana katika awamu sita za makongamano yaliyo fanyika, mji wa Kashiri ni kituo miongoni mwa vituo vya kongamano hilo na linatarajiwa kufika katika miji mingi zaidi ya India, kwa ajili ya kupanua uhusiano zaidi na wapenzi wa Ahlulbait katika kila kona ya India.

Vipengele vya kongamano vitakua kama vifuatavyo:

  • Maonyesho ya vitabu yatakayo fanywa na Ataba tukufu za Iraq.
  • Kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani kama ilivyo kua ikifanyika miaka ya nyuma, chini ya wasomaji wa kimataifa kutoa katika Ataba tukufu.
  • Kutembelea misikiti, husseiniyya, vituo vya kulea mayatima na viongozi wa dini.
  • Kufanya mashindano ya kiitikadi kama inavyo fanyika kila mwaka.
  • Kutoa mihadhara kuhusu utukufu wa Amirul Mu-uminina (a.s).
  • Kufanya vikao vya kitafiti kuhusu utukufu wa Amirul Mu-uminana (a.s) katika chuo kikuu cha Kashmiri, kutakua na mada za kihauza na kisekula.

Pamoja na vitu vingine vingi vinavyo endana na utukufu wa kongamano hilo.

Kamati ya maandalizi ikaendelea kusema kua pamoja na kutembelea Husseiniyya ya Ayatullahi Yusufu tutatembelea sehemu zingine pia, na itakua ni sehemu ya vipengele vya kongamano.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) hufanywa kwa ajili ya kuwaadhimisha Ahlulbait (a.s) na kusambaza utamaduni wao na mwenendo wao wa haki pamoja na historia yao tukufu ambayo imeifundisha dunia maana halisi ya uislamu sambamba na kuonyesha nafasi ya Ataba tukufu za Iraq katika kufanya makongamano, nadwa na mikutano ndani na nje ya Iraq, wakiwa wamefungua mlango wa mawasiliano ya moja kwa moja na jumuiya tofauti, na kufafanua hatua za ujenzi wa Ataba hizo na idara za uongozi walizo nazo na kwa namna gani kwa muda mfupi zimekua minara ya uongofu na mfano bora katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: