Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yapokea waombolezaji…

Maoni katika picha
Mji mtukufu wa Karbala unashuhudia makundi makubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara na mawakibu za waombolezaji, zinazokuja kuomboleza kifo cha mama mtukufu Ummul Banina (a.s) katika kaburi la mtoto wake na tulizo la macho yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hivi ndio walivyo zowea kufanya waumini na wamenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kuomboleza msiba huu, kutokana na nafasi kubwa aliyo nayo mama huyu mtakasifu katika nyoyo za waumini, kilele cha kumbukumbu ya msiba huu hakiishii katika kuongezeka idadi ya mazuwaru peke yake, bali kuna ongezeko kubwa la mawakibu za waombolezaji zinazo kuja kutoka miji tofauti ya Iraq, ndani ya siku mbili yameingia makumi ya mawakibu na misafara ya waombolezaji ndani ya malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbadi (a.s) kuja kuwapa pole.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadhu Ni’imah Salmani ambacho kinahusika na kuratibu matembezi ya mawakibu, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Zimeingia mawakibu nyingi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, sambamba na ujio wa mawakibu za kutoa huduma ya chakula na maji kwa mazuwaru watukufu”.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake imepanga kuhakikisha ziara hii inafanikiwa na kumpatia kila anacho hitaji zaairu mtukufu, pamoja na kurahisisha uingiaji na utokaji wa mawakibu za waombolezaji ndani ya haram tukufu ya Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: