Amani iwe juu yako ewe mama wa mwezi ung’aao, ewe Fatuma binti Hizamu Kilabiyya, uliye pewa jina (laqabu) ya Ummul Banina na Baabul Hawaaiji, tunashuhudia kwa Mwenyezi Mungu na mtume wake hakika wewe ulipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, ulipo jitolea watoto wako kwa ajili ya Hussein mtoto wa binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu…
Katika kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha mtakasifu Ummul Banina (a.s), katika maombolezo ambayo yamezoweleka kufanywa na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, baada ya Adhuhuri ya siku ya Jumanne ya tarehe (13 Jamadal Thani 1440h) sawa na (19 Februari 2019m) watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kusimama na kufanya maombolezo maalumu pamoja na kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) walipokea maukibu ya watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu na kwa pamoja wakampa pole Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya malalo yake takatifu, wakaimba kaswida na kusoma tenzi zilizo amsha hisia za huzuni kutokana na msiba huu.
Fahamu kua wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanafanya maombolezo ya msiba huu, Ummul Banina (a.s) ni miongoni mwa wanawake bora kielimu na kiuchamungu, pamoja na kua alikua mke wa kiongozi wa waumini (a.s) Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) na ni mama wa mnyeshaji wenye kiu Karbala na kamanda wa jeshi la Hussein (a.s) na mbeba bendera yake Abulfadhil Abbasi mwezi wa bani Hashim (a.s).