Baada ya kumaliza uchujaji: Kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwa yatangaza majina ya walio faulu kushiriki katika shindano la utafiti…

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza kuchuja mada zitakazo shiriki katika shindano la utafiti ambalo ni miongoni mwa vipengele vya kongamano la kitamaduni Ruhu Nubuwa ambalo linaandaliwa na Idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kamati ya maandalizi imetangaza majina ya washindi ambao tafiti zao zimekidhi vigezo na masharti ya kongamano.

Kamati ikasema kua tafiti zilizo shinda zitawasilishwa katika vikao vya kongamano, kuhusu tafiti ambazo hazikufaulu lakini zikapata alama za juu zitachapishwa katika toleo maalumu la kongamano.

Walio shinda na kupata nafasi ya kuwasilisha tafiti zao katika kikao cha ufunguzi wa kongamano ni hawa wafuatao:

  • - Mkufunzi Samana Abdul-Azizi: kutoka chuo kikuu cha Karbala/ kitivo cha uongozi na uchumi.
  • - Ustadhat Wasan Swahibu Idaani: kutoka Atabatu Alawiyya tukufu.
  • - Mtafiti Dina Fuadi Jawadi Hassan.

Walio shinda katika shindano maalum la utafiti kwa wanafunzi wa shule za Alkafeel cha wasichana ni hawa wafuatao:

  • - Watafiti wawili, Fatuma Ridhwa na Ruaiy Majidi.
  • - Mtafiti Ghufrani Awadi Sawadi.
  • - Mtafiti Imani Hussein Alawi.

Kumbuka kua lengo la kongamano hili ni kubainisha utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) katika kila sekta, na kutoa pazia kuhusu mchango wake kielimu kupitia tafiti zitakazo wasilishwa, sambamba na kuzipatia maktaba vitabu vinavyo mzungumzia mama huyu mtakasifu na athari yake katika jamii, kwa kuonesha turathi za mbora wa wanawake wa duniani (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: