Kwa namna gani Ummul Banina (a.s) alikua mlango wa haja kwa waumini?

Maoni katika picha
Miongoni mwa wanaojulikana kama mlango wa haja (baabu hawaaiji) na sio katika Maimamu watakasifu (a.s) ni Ummul Banina (a.s) mama wa Abulfadhil Abbasi (a.s) Fatuma binti Hizaam Alwahidiyya Alkilabiyya, alipata utukufu huo kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kutokana na imani nzuri aliyokua nayo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, pamoja na ikhlasi na mapenzi makubwa aliyo kua nayo kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), aliweka nadhiri katika nafsi yake ya kuwatumikia watoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Maimamu watakasifu Hassan na Hussein (a.s), aliwathamini zaidi ya nafsi yake na watoto wake, na akawafundisha watoto wake wawapende kwa dhati, akawapa malezi ya kuwapenda zaidi na kuwa tayali kujitolea nafsi zao kwa ajili yao, na aliwatuma waende pamoja na Imamu wao Hussein (a.s), alipo ondoka Madina kwenda Maka na baadae kwenda Iraq, akawaambia wawe tayali kumnusuru na kujitolea kwa ajili yake, akawahusia wasione tabu kujitolea roho zao kwa ajili ya kumlinda Imamu Hussein (a.s).

Walifanya hivyo, hawakuzembea katika kumnusuru Imamu wao, hawakutanguliza nasfi zao zaidi ya nafsi yake, Ummul Banina alipokutana na mtu kutoka katika msafara wa Imamu Hussein (a.s) hakuuliza hali ya watoto wake bali aliuliza hali ya Imamu Hussein (a.s), kila alivyo kua akiambiwa taarifa ya kuuwawa kwa watoto wake mmoja baada ya mwingine alikua anaitika kwa utulivu, yote hiyo ni kuonyesha namna alivyo jitolea kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s).

Kisha akasema: Nakuuliza kuhusu hali ya Imamu Hussein (a.s) wewe unaniambia kuhusu watoto wangu?! Alipo ambiwa Imamu Hussei (a.s) ameuwawa, alilia sana akaanguka na kupoteza fahamu.

Hapa ilionekana wazi ikhlasi yake na upendo mkubwa alionao kwa Imamu (a.s), maneno yake yanaendana na vitendo vyake, Mwenyezi Mungu amempa utukufu duniani na akhera, na akamfanya kuwa miongoni mwa milango za wenye haja kwake, na njia miongoni mwa njia za radhi na msamaha wake, mtu yeyote atakaye muomba Mwenyezi Mungu kupitia mama huyu mtakasifu Mwenyezi Mungu atakidhi haja yake na kumtatulia tatizo lake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: