Kwa picha: Kazi ya kukarabati maraya kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inaendelea…

Maoni katika picha
Mapambo na nakshi nzuri zilizo sanifiwa na watalamu wa idara ya maraya (marumaru za vioo) chini ya kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu; hii ni sehemu ya pekee katika safari ya ujenzi unao shuhudiwa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi ya kubadilisha maraya katika haram bado inaendelea, uzuri wake unaonekana wazi kwa kila anayeingia katika hara tukufu, kutokana na umakini unaohitajika, kazi hii inahitaji muda ili ionekane katika uzuri wake halisi unao endana na utukufu wa mwenye malalo.

Kuhusu hatua za mradi huu, mtandao wa Alkafeel umeongea na Ustadh Hassan Saidi Mahadi kiongozi wa idara ya maraya katika kitengo cha uangalizi wa kihandisi, ambaye amesema kua: “Tumeanza hatua hii katika kazi ya mradi wa kubadilisha na kurekebisha maraya katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuanzia upande wa mlango wa Imamu Muhammad Jawaad (a.s), kazi hiyo imejumuisha utowaji wa maraya zilizo haribika pamoja na kuondoa chokaa na vifuniko vilivyo haribika”.

Akaongeza kua: “Tulifanya kazi za awali pia kama vile kuweka lea ya chuma kwenye ukuta pamoja na kuweka vitu vinavyo ulinda na unyevunyevu, ili kuufanya uwe imara zaidi, kisha tukaanza kuweka maraya, sio hivyo tu, kuna kazi zingine zinafanyika sambamba na kazi ya maraya, kazi hizo zinafanywa na idara ya umeme ambayo ipo chini ya kitengo chetu”.

Akaendelea kusema: “Kazi bado inaendelea hadi tumalize kubadilisha na kurekebisha maraya zote zilizopo katika haram tukufu, sambamba na kulinda muonekano wa zamani”.

Kuhusu aina na vipimo vya maraya amesema kua: “Tunatumia maraya zinazoitwa (Taiwan), zina muundo wa vifuniko na ukubwa wa (sm180 x 120) na unene wa (mlm 2), hii ndio aina bora zaidi iliyopo katika soko la Iraq, tumechagua rangi inayo endana na eneo husika”.

Kumbuka kua idara ya maraya na nakshi inahusika na kazi ya maraya ndani na nje ya haram tukufu, huweka na kukarabati kitaalamu kwa mikono ya wairaq halisi, ina timkazi maalumu na kuifanya Atabatu Abbasiyya isitegemee watu wa nje kuja kufanya kazi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: