Aina zenye ubora wa hali ya juu: Idara ya vitalu vya Alkafeel yaja na aina mora za mbegu za miti ya matunda kwa wakulima na wananchi…

Maoni katika picha
Kutokana na kuingia msimu wa kupanda miti, idara ya vitalu vya Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasuyya tukufu imetangaza uwepo wa aina bora za mbegu za miti ya matunda zinazo endana na hali ya hewa ya Iraq, inawafaa sana wakulima na wananchi kwa ujumla.

Mbegu hizo zimeandaliwa kwa umakini mkubwa kuanzia katika chanzo chake na kuzileta kwenye kitalu ambapo zimewekewa mbolea stahili na sasa zipo tayali kwa kupandwa, mbegu zenyewe ni:

  • - Mbegu za matunda makali kama vile; limao, ndimu, machungwa, machenza nk.
  • - Mbegu za matunda baridi kama vile; kongamanga, peasi, tufaha nk.

Idara imesema kua mbegu hizo zinapatikana kwenye vituo vyote vya mauzo, ambavyo ni:

Kituo cha kwanza: Karbala kitongoji cha Husseiniyya karibu na Qantwara nyeupe.

Kituo cha pili: Barabara ya Jamhuri karibu na kituo cha ulinzi wa raia.

Kituo cha tatu: Katika jengo la kibiashara Al-Afaaf kwenye mtaa wa Hussein (a.s).

Kwa maelezo zaidi piga simu ifuatayo (07718003738).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: