Mbolea ya (Smart Fart) kutoka shirika la Aljuud ni mbadala bora wa mbolea ya kuweka ardhini…

Maoni katika picha
Mbolea zinazo tengenezwa na shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inaubora wa hali ya juu, inastawisha mimea katika hatua zote, ubora wake umethibitika maabara na shambani, watalamu wa shirika walibaini changamoto zote kisha wakaja ma majibu ya changamoto hizo, miongoni mwa utatuzi wa changamoto hizo ni utengenezwaji wa mbolea hii ya (Smart Fart) mbolea ya maji yenye ubora wa kimataifa kwa asilimia (%100) inayo tumika kwa kupuliziwa kwenye majani, ni mbolea iliyo tengenezwa kwa malighafi za majani ya baharini, wakulima wengi wanaitumia kutokana na uwezo mkubwa iliyo nao wa kustawisha mimea.

Miongoni mwa sifa za mbolea hii ni:

  • Inakiwango kidogo cha madini chumvi.
  • Inakiwango kidogo cha HP6.
  • Inayayuka kwa asilimia (%100) kwenye maji.
  • Haina chembe chembe za Sodyum na koluur.
  • Inafyonzwa kwa urahisi ma mimea.
  • Inatumika kwa kupuliziwa kwenye majani ya mimea.

Upekee wa mbolea hii ni:

  • - Inauwezo mkubwa wa kuongeza kiwango cha uzalishaji.
  • - Inafaa kutumika katika hatua tofauti za ukuwaji wa mimea.
  • - Inauwezo mkubwa wa kuchanganyika na vimiminika vingine vinavyo tumika kwenye mimea.
  • - Inatumika kwenye mimea ya aina tofauti na kote inafanya kazi vizuri.
  • - Ni mbadala bora wa mbolea ya kuweka ardhini.
  • - Inafanya kazi kwa haraka katika mmea mdogo au mkubwa.

Kumbuka kua mbolea hii imetengenezwa na raia halisi wa Iraq na imefanyiwa majaribio mbalimbali na yote imetoa matokea mazuri na kuthibitisha ubora wake, mbolea hiyo inapatikana katika vituo vya mauzo vilivyo chini ya shirika ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwa maelezo zaidi piga namba za simu zifuatazo: (07801930125 / 07801035422) au tembelea kituo cha uhusiano cha shirika kilichopo barabara ya (Karbala / Najafu) mkabala na nguzo namba (1145).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: