Chini ya viwango vya kisasa zaidi kimataifa: Ujenzi wa kitivo cha famasia cha chuo kikuu cha Alkafeel umekamilika…

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilika kwa ujenzi wa kitivo cha famasia cha chuo kikuu cha Alkafeel, ambacho ni moja ya vitivo hai vinavyo toa mafunzo hivi sasa, kinacho tarajia kuhamia katika jengo hilo jipya lililopo katika mkoa wa Najafu Ashrafu katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (8000).

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhwiyaau Majidi Swaaigh, amesema kua: “Tumezingatia viwango vya kimataifa katika sehemu zote za jengo hili vinavyo kubalika na wizara ya elimu ya juu, jengo hili litakapo kamilika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) litakua la kupigiwa mfano katika mkoa wa Najafu Ashrafu, ubora wa jengo hili unaonekana katika sehemu iliyo kamilika hivi karibuni ya kitivo cha famasia, ujenzi huu umefanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, katika ubora sawa au zaidi ya vyuo sawa na hiki vya kimataifa, kwa kiasi ambacho lina mazingira bora ya kujisomea kwa wanafunzi wa chuo au wakufunzi”.

Kuhusu sifa za jengo hilo amesema kua: “Jengo la kitivo cha famasia limejengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1700), lina ghorofa tano, lina kumbi za madarasa, vyumba vya ofisi, maabara, na kumbi za mikutano, kama ifuatavya:

  • - Kuna kumbi nne za madarasa zinazo endana na idadi ya wanafunzi, zina vifaa vyote vya kusomeshea pamoja na vifaa vya kielektronik vya kisasa.
  • - Kuna maabara tisa zilizo wekwa aina zote za vifaa vya maabara vinavyo hitajika na muwezesha mwanafunzi kusoma kwa nadhariyya na vitendo.
  • - Eneo lililobaki nina maktaba na matawi ya idara za watumishi”.

Akaendelea kusema kua: “Katika ujenzi huu tumetumia vifaa vya kisasa na rafiki kwa mazingira vilivyo sanifiwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na vinavyo afikiana na masharti ya wizara ya elimu ya juu”.

Fahamu kua jengo hili la chuo kikuu cha Alkafeel lipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake, jengo hili lina faida zifuatazo:

  • - Kulea akili za wairaq na kuweka mazingira ya kunufaika nazo.
  • - Kupunguza msongamano katika vyuo vya serikali na vyuo binafsi.
  • - Kwendana na maendeleo ya kielimu kinadhariyya na kivitendo, kupitia selebasi na vifaa vya kisasa.

Kumbuka kua jengo hili lipo katika mkakati maalumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, unao lenga kuinua sekta ya elimu hapa Iraq, na kutufanya twende sambamba na maendeleo ya dunia katika sekta hii, baada ya kumaliza hatua za usajili wa taasisi za kimalezi na kielimu, sasa hivi tunaziwezesha taasisi hizo kufanya majukumu yake, moja ya vitu muhimu ni kuwa na majengo yanayo endana na taasisi hizo, huu ni mwanzo wa kuelekea katika njia sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: