Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, Alfajiri ya Jumapili (16 Jamadal Thani 1440h) sawa na (24 Februari 2019m) kimetangaza kuanza msako mkali wa kusafisha mabaki ya magaidi katika jangwa la magharibi waliofanya mauwaji siku chache zilizo pita kwa raia wema waliokua wanajitafutia riziki.
Uongozi umesema katika taarifa waliyo toa kwa vyombo vya habari, katika kuungana na familia zote za mashahidi unafanyika msako huu katika eneo lenye ukubwa wa kilo meta 450, kuanzia upande wa Ambaar hadi jangwa la Ghadafu na kuelekea hadi kwenye mpaka wa Iraq kwa mujibu wa taarifa tulizo pata, wakafafanua kuwa lengo kuu la msako huu ni kusafisha jangwa la Ghadafu na mabaki ya magaidi.
Akabainisha kua msako huu unaongozwa na kikosi cha Ambaar pamoja na kikosi cha Abbasi brugedi ya tano, wamepata ruhusa ya kupanua msako katika jangwa hilo kutoka katika kikosi maalumu cha muungano, wakasema kuwa msako utaendelea hadi watakapo fikia malengo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.