Shekh Adi Kadhimiy: Atabatu Abbasiyya tukufu imechangia kufikisha ujumbe wa Ahlulbait (a.s) na kusambaza elimu yao kwa wapenzi wao na kongamano la Amirul Mu-umina ni moja ya mchango huo…

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu Shekh Adi Kadhimiy amesema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya ni moja ya Ataba zenye mchango mkubwa katika kutangaza mapenzi na elimu ya Ahlulbait (a.s), na wala sio Iraq peke yake, daima imekua mstari wa mbele katika kutangaza elimu ya Ahlulbait kila sehemu ya dunia, na kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s) ambalo hufanywa kila mwaka nchini India ni moja ya kazi hiyo”.

Ameyasema hayo baada ya kupokea mwaliko rasmi ulioletwa katika Atabatu Kadhimiyya kutoka kwa Atabatu Abbasiyya wa kwenda kushiriki katika kongamano litakalo fanyika katika jimbo la Kashmiri nchini India chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirul Mu-uminina (a.s) ni njia iliyo nyooka na kamba madhubuti ya Mwenyezi Mungu), litakalo fanyika mwezi (13 – 17 Rajabu 1440h).

Akaongeza kusema kua: “Kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina ambalo hufanywa kila mwaka nchini India ni moja ya njia za kufikisha ujumbe wa Ahlulbait (a.s), na kuwapa moyo wa kushikamana zaidi na Ahlulbait (a.s) watu wa huko sambamba na kuwafikishia harufu nzuri ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema: “kutokana na makongamano yaliyo fanywa miaka ya nyuma, na taarifa tulizo pata kutoka kwa watumishi wa Atabatu Kadhimiyya walio shiriki katika makongamano hayo zinafurahisha sana, na zinatia moyo wa kuendelea kufanyika kongamano hili kila mwaka, lenye lengo la kuwaunganisha wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na Ataba tukufu, ukizingatia kua ndio chimbuko la masomo ya kiitikadi na kimaadili chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu adumishe jambo hili na awatie nguvu wasimamizi wa kongamano hili na ajaalie ujumbe wa Ahlulbait (a.s) uwe juu, tuweze kuwaonyesha watu wengine ukarimu wao na mwenendo wao (a.s), sisi wote tupo chuni ya kuwatumikia Ahlulbait (a.s), hasa kongamano hili ni muhimu katika kuwatumikia Ahlulbait na kufikisha ujumbe wao”.

Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliokwenda kupeleka mwaliko umeongozwa na Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri Naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye alitoa maelezo kwa ufupi kuhusu kongamano la mwaka huu, pamoja na kuomba ushiriki wa Atabatu Kadhimiyya kwenye kongamano hilo”.

Kumbuka kua kamati ya maandalizi ya kongamano ilitangaza kua maandalizi ya kongamano la mwaka huu yalianza muda mrefu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanaendeleza mazuri yaliyo fanyika katika makongamano yaliyo pita na kuacha athari kubwa katika miji yaliko fanyika (Yalifanyika mara mbili katika mji wa Laknau na yakafanyika katika mji wa Haidar Abaadi na Nakluur iliyopo katika jimbo la Karkata, jambo ambalo limepelekea miji mingine ya India kuleta maombi ya kuwa wenyeji wa kongamano hili, na ndio ukachaguliwa mji wa Kashmiri wa India kuwa mwenyeji wa kongamano hili mwaka huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: