Maoni katika picha
Katika ujumbe waliotoa kwa mtandao wa Alkafeel mkuu wa kikosi hicho Ustadh Maitham Zaidi amesema kua: “Hakika wapiganaji wa kikosi ndani ya muda mfupi wamefanikiwa kusafisha kilometa (500) katika jangwa la mji wa Nukhaib kuelekea jangwa la Ramadi, kikosi kimetumia msako wa kasi katika pande zote, pamoja na kumaliza jukumu tulilopangiwa katika hatua ya kwanza, tutaendelea kufanya msako na kuimarisha ulinzi”
Kumbuka kua msako huu unafanywa chini ya usimamizi wa wizara ya ulinzi ya Iraq kwa kuongozwa na kikosi cha mkoa wa Ambaar pamoja na kikosi cha Abbasi (a.s) blugedi ya 26 ya Hashdi Sha’abi, kikosi cha Abbasi kimewakilishwa na blugedi yake namba tano.