Muhimu… Majemedari wa Alkafeel wavamia eneo la Ghadafu katika jangwa la Gharbiyya

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kikosi cha 26 cha Hashdi Sha’abi umetangaza kua umeingia hatua ya pili katika msako wa safisha safisha mabaki ya magaidi kwenye jangwa la Gharbiyya kwa kuvamia eneo la Ghadafu, eneo ambalo ni moja ya ngome za magaidi wa Daesh wanalo litumia kufanya jinai zao mara kwa mara, chini ya maelekezo ya uongozi wa kikosi cha muungano na msako huu umepewa jina la (kisasi cha wahanga).

Taarifa iliyotufikia katika mtandao wa kimataifa Alkafeel kutoka kwa makamanda wa kikosi cha Abbasi inasema kua Alfajiri ya Jumatatu wameanza hatua ya pili ya msako huo kwa kuvamia eneo la Ghadafu ambalo ni eneo hatari zaidi na hutumiwa kama maficho ya mabaki ya magaidi wa Daesh, taafifa ikathibitisha kuwa wamefikia malengo waliyo kusudia, ya kuimarisha usalama katika jangwa hilo linalo fika hadi mpakani, wakasema kuwa wataeleza kwa urefu mafanikio waliyo pata wakati mwingine.

Kumbuka kua msako huu unafanywa chini ya wizara ya ulinzi ya Iraq na kusimamiwa na kikosi cha Ambaar pamoja na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji brugedi ya 26 ya Hashdi Sha’abi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: