Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dhiqaar inafanya kongamano la Swidiiqatul Kubra (a.s)…

Maoni katika picha
Ukumbi wa mikutano katika kitivo cha (tarbiya lil-uluumi swarfah) kwenye chuo kikuu cha Dhiqaar mwaka wa nane mfululizo unakua mwenyeji wa kongamano la Swidiiqatu Kubra (a.s) linalo simamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambalo ni miongoni mwa mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dhiqaar, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo na wakufunzi sambamba na ugeni ulio wakilisha Ataba tukufu za Iraq.

Kongamano lilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na limedumu kwa muda wa siku tatu, baada ya Qur’ani ya ufunguzi ilisomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq halafu ukasomwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (lahnul-iba).

Halafu ukafuata ujumbe wa rais wa chuo kikuu cha Dhiqaar Dokta Riyaadh Shanata ambaye alisema kua: “Ni fahari kubwa kwetu kufanya kongamano hili kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, watoto wetu wanafuraha sana kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Atabatu Abbasiyya na vyuo vikuu, kwa upande wetu lazima tushirikiane na Ataba tukufu ili tuweze kufikia malengo yetu ya kibinaadamu, kijamii na kitamaduni, kupitia mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na utamaduni wao na fikra zao za pekee”.

Kisha ukafuata ujumbe wa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa kwa niaba yake na Sayyid Adnani Mussawi kutoka kitengo cha Dini, miongoni mwa aliyo sema ni: “Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake kitukufu, (Na msichana aliye zikwa hai atakapo ulizwa* Kwa kosa gani uliuliwa?) kupitia aya hizi nataka kubainisha haki za mwanamke katika uislamu, katika siku hizi za kukumbuka kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s) tunaweza kusema siku hizi zinaumuhimu mkubwa katika katika maisha ya mwanamke…”.

Hafla imepambwa na mashairi kutoka kwa wanachuo, yaliyo zungumzia utukufu wa bibi Zaharaa (a.s), mshairi wa Atabatu Askariyya tukufu bwana Qaswiri Dujaili alisoma tenzi kwa sauti nzuri sana, kuhusu kumpenda bibi Zahara na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s).

Kongamano lilifungwa kwa kugawa midani na vyeti vya ushiriki kwa wanafunzi walioshiriki shindalo lililo fanyika kwenye kongamano hilo.

Baada ya kumaliza kongamano watu walielekea katika ufunguzi wa maonyesho ya vitabu na picha yanayo fanywa na kitengo cha habari na utamaduni kwa kushirikiana na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu na tawi lingine lililokua na vifaa kale kutoka katika makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na tawi maalumu la Atabatu Husseiniyya tukufu, pia kulikua na mjadala wa wazi wa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: