Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) hivi ndio walivyo upokea usiku wa kuzaliwa Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Mabruuk mabruuk kwa kuzaliwa

Mbora wa wanawake wote watakasifu

Usiku wa kuzaliwa kwako tunaukumbuka kwa furaha

Muombezi wa watu duniani na akhera

Tunampongeza kwa furaha Nabii wetu na Haidari

Ni siku ya fursha na nuru inang’aa

Kuzaliwa kwema kwa mridhia na mridhiwa

Kwa beti hizi watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanatoa pongezi kwa umma wa waislamu na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waliobahatika kuja kufanya ziara kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa wanawake wa duniani bibi Hauraa Fatuma Zaharaa (a.s).

Yalisemwa hayo katika program iliyo fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumatatu (19 Jamadal Thani 1440h) sawa na (25 Februari 2019m) ya kusherehekea kuzaliwa kwa Zaharaa Albatuli (a.s).

Baada ya watumishi wa mwezi wa familia kusimama katika mistari na kusoma ziara maalumu pamoja na wimbo wa Atabatu Abbasiyya unaoitwa (Lahnul-iba), walianza kuimba beti nzuri zinazo onyesha ukubwa wa furaha yao kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s), walinyoosha mikono yao ikiwa imeshika mauwa na kuimba kaswida nzuri na kumpongeza Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) na Maraajii watukufu na wakaupongeza umma wa kiislamu kwa kuzaliwa mama wa Maimamu wawili Hassan na Hussein (a.s).

Mwimbaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Yassir Karbalai alionyesha ukubwa wa furaha yake kwa kuimba kaswida maalum kuhusu tukio hili tukufu akasema ni utukufu mkubwa kupata nafasi ya kupongeza kuzaliwa kwa Zaharaa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: