Mwezi ishirini Jamadal Thani dunia iliangaziwa na nuru ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma (a.s)…

Maoni katika picha
Siku ya mwezi (20 Jamadal Thani) ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) pande la damu ya Mtume (s.a.w.w), kuzaliwa kwake kuling’arisha nuru Muhammadiyya Mwenyezi Mungu akaiangazia dunia na akashusha Kauthara.

Kutoka kwa Mufadhil bun Omari anasema: Nilimuuliza Abu Abdillahi Swadiq (a.s): Mazazi ya bibi Fatuma (a.s) yalikua vipi? Akasema: Bibi Khadija alipo olewa na Mtume (s.a.w.w) wanawake wa Maka walimtenga, wakawa hawaingii nyumbani kwake wala hawamsalimii, na hawaruhusu mwanamke yeyote aingie kwake, akawa furaha na huzuni yake ni yeye na Mtume (s.a.w.w) peke yao, alipo pata ujauzito wa Fatuma (a.s), akawa Fatuma anaongea na mama yake akiwa bado yuko tumboni na kumwambia avumilie, alimficha Mtume jambo hilo, siku moja Mtume alipoingia akamkuta bibi Khadija anaongea na Fatuma (ujauzito), Mtume (s.a.w.w) akamuuliza: ewe Khadija unaongea na nani? Akasema: mtoto aliye tumboni mwangu ananizungumzisha na kuniliwaza, akasema: ewe Khadiji huyu hapa Jibriru ananiambia kua mtoto huyo ni mwanamke naye ni mtakasifu, na Mwenyezi Mungu mtukufu ataendeleza kizazi changu kupitia yeye na kizazi chake ndio cha maimamu watakao kuwa viongozi hapa duniani baada ya kuisha wahyi.

Bibi Khadija aliendelea kuwa katika hali hiyo (ya kuongea na ujauzito wake) hadi ulipo fika wakati wa kujifungua, wakafatwa wanawake (wakunga) wa kikuraishi ili waje kumsaidia wakati wa kujifungua, wanawake (wakunga) wakakataa, wakasema: wewe ulituasi haukusikiliza maneno yetu, umeolewa na Muhammad yatima wa Abu Twalib mtu fakiri hana mali, hatuji kukusaidia wakati wa kujifungua, Khadija (a.s) akapata uchungu akiwa peke yake, ghafla wakaingia wanawake wanne warefu kama wanawake wa bani Hashim, akashtuka baada ya kuwaona, mmoja wao akasema: Usihuzinike ewe Khadija hakika sisi ni wajumbe kutoka kwa Mola wako sisi ni ndugu zako, mimi ni Sara na huyu ni Asia bint Muzahim rafiki yako wa peponi na huyu ni Maryam bint Imraan na huyu ni Kulthum dada wa Nabii Mussa bun Imraan, Mwenyezi Mungu ametutuma kuja kukusaidia katika uzazi (kuwa wakunga wako), mmoja akakaa upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto na watatu akakaa mbele yake na wanne akakaa mgongoni kwake, ndipo akazaliwa bibi Fatuma (a.s) mtakasifu akiwa msafi.

Alipo ingia duniani nuru iliangaza hadi katika nyumba za watu wa Maka, mashariki na magharibi kote nuru hiyo iliangaza, kisha wakaingia Mahurain kumi kila mmoja kati yao akiwa ameshika beseni na birika kutoka peponi na katika birika kuna maji kutoka katika mto wa Kauthara, wakapokelewa na yule aliyekaa mbele yake na akamuogesha Fatuma kwa maji yaliyotoka katika mto wa Kauthara, wakatoa vitambaa viwili vyeupe kushinda maziwa na vinaharufu nzuri kushinda miski na ambari, kitambaa kimoja wakamfunga na kingine wakamfunika kisha wakamtamkisha Fatuma (a.s) akatamka shahada mbili, akasema: Nashuhudia kua hakuna Mungu ispokua Allah na hakika baba yangu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mbora wa Manabii na hakika mume wangu ni mbora wa mawasii na watoto wangu ni wajukuu bora, kisha akawasalimia na akamtaja kila mmoja kwa jina lake, wakacheka kwa furaha, watu wakaanza kupeana taarifa ya kuzaliwa kwa Fatuma (a.s), ikawaka nuru kubwa angani ambayo ilikua haijawahi kuonekana, wale wanawake wakasema: Ewe Khadija mchukue mwanao mtakasifu, msafi, mtakatifu amebarikiwa yeye na kizazi chake.

Akamchukua kwa furaha kaubwa na kumkumbatia kifuani kwake, bibi Fatuma (a.s) alikua kwa haraka sana, siku moja kwake ilikua sawa na mwezi mmoja kwa watoto wa kawaida na mwezi mmoja sawa na mwaka mmoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: