Maoni katika picha
Mandhari ya furaha imetanda, kwa kuwekwa mapambo mbalimbali katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na eneo la katikati yao, miongoni mwa mambo yanayo onyesha furaha ni yale yaliyo fanywa na kitengo cha utumishi (kikosi cha vitalu vya Alkafeel) katika Atabatu Abbasiyya, wameweka miti mbalimbali ya mapambo pamoja na mauwa mazuri katika eneo lote linalo zunguka Ataba tukufu, na ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kuna mabango mbalimbali yaliyo andikwa maneno ya pongezi na aya za Qur’ani pamoja na hadithi za Mtume na Ahlulbait (a.s).
Hali kadhalika kuta na nguzo za Ataba tukufu zimepambwa mauwa mazuri yanayo akisi furaha ya waumini katika mnasaba huu, kwa nini isiwe hivyo wakati tunasherehekea kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s).