Katika toleo la uhakiki: Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimekusanya urithi wa maktaba ya Allammah Ayatullahi Sayyid Hassan Swadri…

Maoni katika picha
Miongoni mwa matoleo yake ya uhakiki yanayo enzi turathi za kiislamu, hivi karibuni kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu chenye jina la: (Ibanatul-wasan an maktabati Abi Muhammad Hassan), ambacho ni faharasi ya maktaba ya Ayatullahi Sayyid Hassan Swadri wa mwaka (1354h) faharasi iliyo andaliwa na mwanae Allammah Sayyid Ali bun Sayyid Hassan Swadri Alkadhimi mwaka (1380h), na imehakikiwa na Mheshimiwa Sayyid Jafari Husseini Ashkuuri, ametoa kitabu chenye kurasa (561), ameoredhesha vitabu kwa kufuata utaratibu wa herufi.

Kuhusu kitabu hiki tumeongea na kiongozi wa idara ya usimamizi wa kielimu katika kitengo tajwa hapo juu Shekh Amjad Abduraufu Barqawi amesema kua: “Kutokana na umuhimu wa kutambua umma zilizo pita tunatafuta urithi wao, kupitia urithi huo tunaweza kufahamu kiwango cha utukufu wao”.

Akaongeza kua: “Hakika turathi hujulisha mambo yaliyopita zamani na husaidia kutunza watu wasipoteze mwelekeo wa wazee wao, na wasipoteze historia yao, kwa hiyo ni muhimu sana kuzihifadhi”.

Akasema: “Kitabu hiki kimekusanya urithi mwingi wa vitabu, na kimetuonyesha lulu zilizo kuwepo katika maktaba hiyo, mwenye maktaba alikua mnara wa ushia na alisoma katika mji wa Najafu, Kadhimiyya na Samaraa, alikua mwanachuoni mkubwa sana”.

Kumbuka kua kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vilivyo tolewa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, tunatarajia kitasaidia watafiti wa elimu na kinafaa kwa mustakbali wa masomo yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: