Katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): Beti za mashairi na tenzi muruwa kuhusu kuzaliwa kwa Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Tupo katika siku za kusherehekea kuzaliwa kwa pande ta damu ya Mtume (s.a.w.w) na roho iliyopo katika mbavu zake, mama wa Maimamu Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s).

Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu imefanya hafla ya kuhuisha na kukumbuka kuzaliwa kwa Zaharaa Albatuli (a.s) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hafla ilifanywa Alasiri ya Jumanne (20 Jamadal Thani 1440h) sawa na (26 Februari 2019m) na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mazuwaru waliokuwepo ndani ya haram tukufu.

Rais wa kitengo tajwa hapo juu bwana Riyadh Ni’imah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya huwa kinahuisha matukio yote yanayo husiana na watu wa nyumba ya Mtume ikiwa ni pamoja na kukumbuka kuzaliwa au kufariki kwao, kwani kuhuisha matukio hayo ndio jukumu letu kubwa na ndio urithi mkubwa wa watu wa Karbala”.

Akaongeza kua: “Leo tunasherehekea kuzaliwa kwa Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) mbele ya ndugu zetu watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kundi kubwa la mazuwaru wanashirikiana nasi katika furaha hii ya waumini wote ambao ni wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akabainisha kua: “Halfa inamihadhara mingi pamoja na kaswida mbalimbali za kumsifu bibi Zaharaa (a.s), kutoka kwa waimbaji watotu ambao ni, Salamu Sharufi, Muhammad Haairiy na Ahmadi Shaakiri Ahmadi Karbalai, walifurahisha nyoyo za wahudhuliaji kwa kaswida zilizo imbwa kwa sauti nzuri zilizo elezea utukufu wa Fatuma Batuli (a.s)”.

Fahamu kua kufanya maadhimisho na hafla pamoja na vikao vya taazia na furaha ndio mambo muhimu yanayo fanywa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ata mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kazi yetu haiishii kwenye kuratibu mawakibu peke yake bali huwa tunafanya program mbalimbali za dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: