Maoni katika picha
Hafla ilifanyika katika ukumbi mkuu wa chuo, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Iba).
Halafu ukafuata ujumbe wa rais wa chuo kikuu cha Somar ulio wasilishwa kwa niaba yake na Dokta Abbasi Aqaabi mkuu wa kitivo cha utawala na uchumi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Leo tunapokea ujumbe mtukufu kutoka katika Ataba mbili tukufu unaotupa nuru katika nadwa hii, na upande mwingine wa nadwa ni watoto wetu na wanafunzi wetu watukufu”.
Akaongeza kua: “Wanafunzi watukufu nadwa hii ni ya kitamaduni na kielimu na nyie ni wawakilishi wazuri wa chuo hiki”.
Kisha ukafuata ujumbe wa wageni uliowasilishwa na Sayyid Muhammad Mussawi kutoka katika kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kutoa salamu na kuomba dua akasema kua: “Yatupasa kuangalia nyumba hii takatifu (nyumba ya Ali na Fatuma) haikuwa nyumba ya kawaida hakika ni sawa na chuo kikuu cha kiislamu, na kila mtu anatakiwa asome katika chuo kikuu hicho, ili ajifundishe utaratibu wa familia na malezi bora elimu na ibada kutoka katika nyumba hiyo, hakika masomo yote yanapatikana katika nyumba ya Ali na Fatuma (a.s), kipindi bora alichoishi bibi Fatuma ni kile kipindi kifupi alichokuwa na Imamu Ali (a.s), pamoja na kwamba kilijaa vita na fitina”.
Akaongeza kua: “Hakika nyumba hii tunayo tamani kuwa karibu nayo na kusoma mwenendo wao na hilo ndio jambo muhimu zaidi kwetu, bibi Fatuma alipoenda kwa Imamu Ali tunaona alikua ameweka mbegu ya kuanza maisha katika nyumba yake mpya, ambayo ni mbegu ya mahaba (mapenzi) na hili ni jambo muhimu sana katika maisha ya familia, haitakiwi mapenzi yakosekane katika maisha ya familia, mapenzi ni msingi uliowekwa na Mwenyezi Mungu na aliutekeleza bibi Zaharaa (a.s) katika nyumba ya Ali pamoja na watoto wake, jambo hili limesisitizwa sana na Qur’ani tukufu katika kujenga familia, kanuni ya mapenzi lazima iwe chuoni kwa sababu ukitaka kuyafundisha hautaweza kama hakuna msingi wa mapenzi na utashi, nukta hii ni muhimu sana.
Akaendelea kusema: “Miongoni mwa mambo muhimu aliyokua Zaharaa (a.s) anayafanya ni malezi ya kibinaadamu, ili kujua mambo hayo tunaweza kuangalia riwaya zinazo tuambia namna Hassan na Hussein (a.s) walivyokua wanakaa na jinsi Mtume (s.a.w.w) alivyo kua akiwaambia, Zaharaa (a.s) alikua anambeba Hassan na Hussein na anaenda nao kwa kiongozi wa waumini (a.s) kisha Ali (a.s) anamwambia, wapeleke kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ili awafundishe kitu, maneno hayo yanawajenga kusoma kitu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), baba atakapokua anamsifu mwanae na babu pia akawa anamsifu jambo hilo hujenga kujiamini kwa mtoto, hivyo ndio ilivyokua katika nyumba ya Ali na Fatuma ambayo tunatakiwa kusoma katika nyumba hiyo”.
Akasema: “Kunajambo lingine muhimu, nyumba ya Ali na Fatuma (a.s) ilikua inamalezi bora kiroho, kuanzia siku ya kwanza ya kuzaliwa mtoto, siku aliyozaliwa Hassan na Hussein (a.s) Mtume (s.a.w.w) aliwaadhinia na kukimu katika masikio yao, yaani Mtume mwenyewe aliwafundisha kusoma takbira, hii ni sehemu ya malezi ya kiroho katika nyumba ya Ali na Fatuma, sambamba na sekta ya kielimu katika nyumba yao, bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alitilia umuhimu mkubwa sana katika sekta ya elimu na alikua anawafundisha wakina mama nyumbani kwake”.
Akamaliza kwa kusema: “Tunatarajia kwa wanafunzi wa kiume na wakike wayape masomo umuhimu mkubwa, huo ndio ujumbe kutoka kwa Zaharaa (a.s), na kuna ujumbe wa wazi mwingi kutoka kwake (a.s), hakika Zaharaa alikua mtu wenye kujistiri, mwenye haya, mnyenyekevu, mkarimu, mwenye subira, mpambanaji na mchapa kazi, alikua anatoka pamoja na Mtume (s.a.w.w) kwenda vitani kwa ajili ya kutibu majeruhi, tunamuomba Mwenyezi Mungu ajalie baraka na rehema kwetu katika kumbukumbu hii, aipe umri mrefu sehemu hii na ajaalie iwe msingi wa kila jambo zuri lenye kheri na baraka”.
Baada ya hapo likaanza darasa mjadala (nadwa) kati ya wageni kutoka Atabatu Abbasiyya na wanafunzi wa chuo kikuu cha Somar.
Na mwisho wa nadwa hiyo wageni kutoka Atabatu Abbasiyya wakapewa midani na viongozi wa chuo kikuu cha Somar, pia wageni wakawapa zawadi viongozi wa chuo kutokana na kufanikisha kongamano hili, hali kadhalika kulikua na maonyesho ya baadhi ya machapisho kutoka katika kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.