Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu Dokta Swadiq Muhammad Hamaash katika ujumbe aliotoa kwenye kikao cha ufunguzi amesema kua: “Hakika chuo kikuu cha Mustanswiriyya kilikua na kitaendelea kua chemchem ya elimu, kwa ajili ya kutengeneza jamii yenye maendeleo” akasema: “Kongamano hili ni miongoni mwa siasa za chuo inayo kusudia kuboresha utendaji, na kutufanya twendane na mtazamo mpya wa wizara ya elimu ya juu unao lenga kuleta mapinduzi ya elimu kwa kuweka selebasi za masomo ya kielektronik”.
Naye rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Daokta Abbasi Dida, amesema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inakipongeza chuo cha Mustanswiriyya na vyuo vingine kwa kutumia elimu za kielektronik, na kurahisisha matumizi yake, kwani wamepiga hatua kubwa katika jambo hili na tayali matunda yake yameanza kuonekana”.
Mkuu wa kitivo cha Adabu katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya Dokta Faridah Jaasim Daara amesema kua: “Hakika kongamano linalenga kupata program mpya katika kupangilia na kuweka faharasi, kama program ya (RAD) na kanuni ya (MARC), pamoja na kujadili swala la faharasi katika mazingira ya namba kwenye maktaba za waarabu, na kuangalia namna ya kuboresha ushirikiano katika sekta ya namba kwenye nyanja tofauti za elimu”.
Imepangwa kujadili katika kongamano lenye anuani isemayo: (Kupangilia maarifa kwa namba ndio njia yetu ya maendeleo ya kweli katika usomaji na usomeshaji) litakalo kuwa la siku mbili, siku moja katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya na siku ya pili katika Atabatu Abbasiyya tukufu, litakuwa na tafiti (36) kutoka Uingereza, Iran, Aljeria, Misri, Omaan, Jodan, Lebanon na Palestina, tafiti hizo zimegawanyika sehemu nne: maandalizi ya kisekula katika sekta ya kuratibu namba na kubaini mazingira ya namba, njia za kujua mazingira ya namba, na kuangalia vipimo na kanuni za kisasa pamoja na taasisi za elimu na nafasi yake katika kuratibu maarifa ya namba.
Pembezoni mwa hafla ya ufunguzi wa kongamano ikafunguliwa parua pepe maalumu ya chuo kikuu cha Mustanswiriyya kwa ajili ya kuadhimisha miaka hamsini na tano tangu kuanzishwa kwake, pamoja na kuzindua maonyesho ya vifaa na nakala kale.