Studio ya Aljuud ya picha za katuni inashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu vya watoto yanayo fanyika Karbala…

Maoni katika picha
Pamoja na kwamba inashiriki kwa mara ya kwanza maonyesho ya kimataifa ya vitabu vya watoto hapa Karbala, studio ya Aljuud ya picha za katuni chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imepata mafanikio makubwa katika kushiriki kwake maonyesho haya.

Mafanikio hayo yametokana na kufurahishwa kila aliye tembelea tawi hilo na limekuwa kivutio kikubwa kwa washiriki wote, kutokana na upekee wa vitu wanavyo onyesha ambavyo vimeteka akili za watoto, na vinalea na kukuza uwezo wao kiakili, wanabidhaa za pekee kabisa hapa Iraq zinazo onyesha uwezo mkubwa wa akili na ufundi.

Kiongozi wa Studio Ustadh Ahmadi Twalib Abdul-Amiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Miongoni mwa sababu muhimu za mafanikio haya ni kuifanya studio kuweza kufikiwa na mazuwaru wote pamoja na taasisi mbalimbali na vyombo vya habari, tuna matoleo mengi ya filamu na katuni mbalimbali zinazo saidia kukomaza akili za watoto, tofauti na baadhi ya vyombo vingine vya habari vilivyo enea kila kona ya dunia huonyesha katuni ambazo haziendani na watoto”.

Akaongeza kua: “Tumempa mototo nafasi kubwa katika kazi zetu, kwa lengo la kumfundisha maadili mazuri na kukomaza akili yake, kwa namna ambayo tunamjengea uwelewa wa mambo mengi yanayo mzunguka, malengo ya katuni zetu ni kuwajenga watoto kimaadili kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya kiislamu”.

Kumbuka kua ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu haujaishia katika tawi la studio peke yake, bali kulikua na matawi mengine yaliyo shiriki ya idara za watoto na makuzi zikiwa na machapisho mengi ya watoto wa rika zote, matawi hayo yamepata mwitikio mkubwa kutoka kwa watu waliokuja kutembelea maonyesho haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: